IQNA

11:42 - May 23, 2022
Habari ID: 3475283
TEHRAN (IQNA)-Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema maadui wa mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena wamedhihirisha dhati ya shari yao kwa ugaidi na kumuua shahidi mmoja kati ya askari wa IRGC.

Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) jana ilitangaza kuwa mmoja wa askari wake ambaye ni Mlinzi wa Haram ameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi mjini Tehran Jumapili jioni. Kwa mujibu wa taarifa ya IRGC, askari mwenye kuheshimika mlinzi wa Haram Kanali Hassan Sayyad Khodaei aliuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya wapinga Mapinduzi ya Kiislamu na maajenti wa madola ya kiistikbari duniani.

Taarifa ya IRGC imeongeza kuwa: "Leo (Jumapili) katika moja ya vichochore vinavyoelekea Barabara ya Mujahidina Islam mashariki mwa Tehran, mlinzi wa Haram, Kanali wa IRGC Sayyad Khodaei amelengwa katika jinai ya kigaidi ya walio dhidi ya Mapinduzi ambao ni maajenti wanaofungamana na uistikbari wa kimataifa."

IRGC imetuma salamu za pongezi  sambamba na rambirambia kwa familia ya Kanali Khodaei na kusema: "Hatua za lazima zimechukuliwa kwa ajili ya kutambua na kukamata mhusika au wahusika wa jinai hiyo."

Shahidi Sayyad Khodaei ameuawa shahidi wakiwa ndani ya gari lake mbele ya nyumba yake,

Katika taarifa Jumapili usiku, Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alituma salamu za pongezi na rambimbi rambia kwa familia ya Shahidi Sayyad Khodaie.

Aidha amelaani vikali oparesheni ya kigaidi iliyopelewa kuuwa shahidi Luteni Khodaei na kusema jinai hii dhidi ya binadamu imetekelezwa na uistikbari wa kimataifa. Halikadhalika amebainisha masikitiko yake kuwa nchi za Magharibi zinazodai kukabiliana na ugaidi zimenyamazia kimya na kuunga mkono jinai hiyo.

Amesema katika kipindi cha miongo minne Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa mhanga wa ugaidi na kuongeza kuwa magaidi wanadhana batili kuwa vitendo vyao vitapelekea taifa adhimu la Iran lishindwe kufikia malengo yake ya juu na kusitisha mchakato wa izza na heshima wa watu wa nchi hii lakini wameghafilika kwani hawafahamu kuwa damu ya mashahidi ndiyo inayodhamini kubakia na kufika daraja la juu taifa hili.

Wakati huo huo, tovuti ya Nour News, iliyo karibu na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, imechapisha taarifa katika ukruasa wake wa Twitter na kutaja hatua ya mauaji ya Shahidi Khodaei yalikuwa kuwa iliyo na "ni kuvuka mstari mwekundu jambo ambalo litabadilisha mahesabu mengi." Aida taarifa hiyo imesema waliopanga mauaji hayo na waliyoyatekeleza watapata adhabu kali.

3479013

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: