IQNA

Waislamu Sri Lanka hawaendi Hija mwaka huu kutokana na matatizo ya kiuchumi

12:04 - June 02, 2022
Habari ID: 3475326
TEHRAN (IQNA)- Mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi unaoikabili Sri Lanka iliyokumbwa na madeni umewalazimu Waislamu kutotekeleza ibada ya Hija mwaka huu.

Saudi Arabia ilikuwa imeidhinisha kiwango cha Mahujaji 1,585 kutoka Sri Lanka kwa mwaka wa 2022. Hata hivyo, iliamuliwa kwamba hakuna Mwislamu yeyote kutoka Sri Lanka ambaye antasafiri kwa ajili ya Hija wakati huu, kufuatia majadiliano yaliyofanywa na pande kadhaa ikiwa ni pamoja na Kamati ya Kitaifa ya Hijja, Jumuiya ya Waendeshaji Ziara ya Hajj ya Sri Lanka, na Idara ya Masuala ya Dini na Utamaduni ya Kiislamu.

"Wakati wa kutathmini  hali iliyopo na masaibu wanayopata watu wa Sri Lanka, wanachama wa vyama vyote viwili waliamua Waislamu wasitekeleza Ibada ya Hija ya mwaka huu," ilisema barua iliyoelekezwa kwa Idara ya Masuala ya Kidini na Utamaduni ya Waislamu na Jumuiya ya Mashirika ya Safari za Hija  Sri Lanka.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mashirika ya Safari za Hija  Sri Lanka Rizmi Reyal, wakati huo huo, alisema uamuzi wa wasimamisi wa Hija nchini humo  ulikuwa wa kauli moja kutokana na mgogoro mkubwa wa kicchumi ambao umepelekea kuwepo uhaba mkubwa dola nchini humo.

Sri Lanka imekuwa ikikabiliwa na mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1948, kwa kiasi fulani kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni, ambayo ina maana kwamba nchi hiyo haina uwezo wa kulipia uagizaji wa vyakula vikuu na mafuta ya petroli, jambo ambalo limesababisha ujaba mubwa wa bidhaa na mfumuko mkubwa wa bei.

"Operesheni nzima ya Hija ya mahujaji wa Sri Lanka itagharimu karibu dola milioni 10, na hicho ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na hali ya sasa ya uchumi wa nchi," amesema Ahkam Uwais, mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Hija chini ya Idara ya Masuala ya Kidini ya Kiislamu ya Sri Lanka.

"Uamuzi wa kuacha Hija ya mwaka huu ni ishara ya ukarimu ya wanachama wa jamii ya Kiislamu kujitolea kuhiji kwa ajili ya nchi," aliongeza.

Waislamu ni karibu asilimia 10 ya watu milioni 22 wa Sri Lanka  ambao wengi wengi wao ni Wabudha.

/3479150

captcha