IQNA

Ibada ya Hija

Wairani waanza safari ya kutekeleza Ibada ya Hija

13:07 - June 12, 2022
Habari ID: 3475368
TEHRAN (IQNA)-Kundi la kwanza la Waislamu wa Iran wanaokwenda kutekeleza ibada tukufu ya Hija limeondoka Tehran leo asubuhi kwenda katika mji mtukufu wa Madina nchini Saudi Arabia.

Akihutubu katika hafla ya kuwaaga wageni hao wa Mwenyezi Mungu, Sayyid Sadeq Hosseini, Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria miongozo iliyotolewa hapo awali na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu Hija ya mwaka huu.

Aidha ametoa wito kwa mahujaji kuzingatia kanuni za kiafya za COVID-19 kwani ugonjwa huo bado ni tishio kwa jamii.

Jumla ya Wairani 39,635 watakwenda kutekeleza ibada tukufu ya Hija mwaka huu, wakitokea kwenye viwanja 17 vya ndege vya Jamhuri ya Kiislamu.

Leo ndege zingine nne zitaondoka Iran zikielekea Saudia zikiwa zimewabeba Mahujaji.

Saudi Arabia ilitangaza kuwa itawaruhusu Waislamu milioni moja kutoka ndani na nje ya nchi kushiriki katika Hija mwaka huu, hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi baada ya vizuizi vya janga la Corona kulazimisha kupunguzwa idadi ya mahujaji katika kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Hivi sasa kuna Wairani milioni 5.8 ambao wamejisajili kutekeleza Ibada ya Hija na kwa miaka kadhaa wamekuwa wakisuburi zamu yao.

 4063562

Kishikizo: hija iran saudi arabia
captcha