IQNA

Waziri Mkuu wa Malaysia

Waislamu warejee katika muujiza wa Qur’ani Tukufu ili kuwa na umoja

19:00 - July 01, 2022
Habari ID: 3475445
TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Malaysia Ismail Sabri Yaakob amewasihi Waislamu kurejelea Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW kama miongozo wakati wa kushughulika na kutokuelewana.

Alisema tofauti za maoni lazima zishughulikiwe kwa njia ya heshima na ya maadili, na kuongeza kuwa ukosefu wa umoja unaweza kushughulikiwa ikiwa Waislamu watarejea kwenye mafundisho ya msingi zaidi kwa kushikamana na Qur’ani na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW

"Muujiza wa Qur’ani, kwa ujumla, unaangazia roho ya umoja," Yaakob alisema.

Alitoa maoni hayo katika hotuba yake wakati akiongoza katika Mkutano wa Maulamaa wa Kusini wa Asia ya Kusini 2022 huko Petaling Jaya mnamo Alhamisi (Juni 30).

Pia waliohudhuria walikuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Masuala ya Kidini) Idris Ahmad na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu Sheikh Muhammad Abdul Karim al-Issa.

Wajumbe wa kidini kutoka mataifa 17 walishiriki katika mkutano huo, ambao unafanyika kwa mara ya kwanza.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu pia aligusa juu ya suala la matamshi ya dharau juu dhidi ya Nabii Muhammad (PBUH) nchini India, ambayo alielezea kama kitendo cha uchochezi ambacho kilitishia maelewano ya jamii yake (India) ya dini nyingi.

Ismail Sabri alisema tukio hilo sio tu lilisababisha maandamano ya Waislamu nchini India, lakini pia maeeneo yote duniani, Malaysia ikiwemo.

"Kumtusi Nabii Muhammad (SAW) ni kosa kubwa sana na Waislamu wanapaswa kukabiliana na uovu huo kwa mujibu wa mafundisho ya kidini.”

Amesema katika kukabiliana na vitendo hivyo vya chuki Waislamu hawapaswi kutumbukia katika mtego wa walo ambao wanataka kusababisha uhasama kati ya wafuasi wa dini mbali mbali duniani.

Ismail Sabri pia alilaani udhalimu wa utawala wa Kizayuni wa Israel  ambao unaendelea kuwakandamiza na kuwauwa Wapalestina.

3479525

captcha