IQNA

Ibada ya Hija na kadhia ya Palestina

Mahujaji wahudhuria Mkutano wa Makka kuhusu Palestina, Wajibu wa Umma wa Kiislamu

17:23 - July 05, 2022
Habari ID: 3475463
TEHRAN (IQNA) - Kongamano kuhusu kadhia ya Palestina na wajibu wa Umma wa Kiislamu kuhusu Palestina lilifanyika katika mji mtakatifu wa Makka.

‘Ofisi ya mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Hija iliandaa hafla hiyo siku ya Jumatatu kwa kushirikisha Mahujaji kutoka nchi mbalimbali.

Hujjatul Islam Abdol Fattah Navab, mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Hija, katika ujumbe wake kwenye mkutano huo amesisitiza juu ya ulazima wa kuwekwa wazi hatari za kiutamaduni, kisiasa na kijeshi za kuhalalisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani katika njama hiyo ya kuzishinikiza nchi za Kiarabu zinzishe uhusuano ramsi na utawala bandia wa Israel.

Vile vile ameitaja Hija kuwa ni dhihirisho la umoja wa Kiislamu na kusema Hija ni ibada pekee inayoweza kuutia moyo Umma wa Kiislamu katika mchakato wa kuhuisha maadili ya Kiislamu na kukabiliana na maadui.

Hujjatul islam Navab ameashiria msisitizo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kudumisha umoja na kusema kunapaswa kuweko mipango ya kina na hatua zichukuliwe ili kubainisha umuhimu wa umoja na mafungamano na vitisho vya hitilafu na mifarakano.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shirika la Hija la Iran Seyed Sadeq Hosseini alikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo. Amefafanua juu ya ulazima wa kukuzwa kadhia ya Al-Quds (Jerusalem) na kuongeza ufahamu kuhusu yale wanayopitia wananchi wa Palestina.

Kwingineko katika mkutano huo idadi ya wasomi na wanafikra kutoka Uturuki, India, Pakistani na Niger waliwasilisha maoni yao juu ya jukumu la Umma wa Kiislamu katika kutetea Palestina.

Takriban mahujaji milioni moja kutoka nchi mbalimbali wako mjini Mecca kutekeleza ibada ya Hija.

 

4068602

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :