IQNA

Ibada ya Hija na Umrah

Waziri Mkuu wa Iraq atekeleza Hija ndogo ya Umrah akiwa ziarani Saudia

23:09 - June 26, 2022
Habari ID: 3475429
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Iraq Musafa al Kadhimi ametekeleza Hija ndogo ya Umrah akiwa katika ziara rasmi nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa taarifa, Al-Kadhimi na maafisa waliokuwa katika ujumbe wake walitekeleza ibada ya Umrah Jumapili asubuhi. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq imechapisha picha za Al Kadhimi akiwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makka akitekeleza amali za Umrah. Al Kadhimi aliwasili Jeddah Jumamosi jioni na kulakiwa na mrithi wa ufalme wa Saudia, mwanamfalme Mohammad bin Salman ambaye kivitendo hivi sasa ndie kiongozi wa ufalme huo. Baada ya kukamilisha safari yake Saudia, Al Kadhimi ameelekea Iran ambapo Jumapili alasiri amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Ebrahim Raeisi mjini Tehran.

Hija za Umrah ni ibada inayojumuisha safari ya kuelekea Makka ina ina amali kama vile ihram, kutufu al Kaaba , kutembea baina ya milima ya Safa na Marwah na kunyoa nywele. Amali hizi za kimsingi ambazo hutekelezwa katika Umrah ambayo pia huitwa Hija ndogo ambayo inaweza kufanyaika wakati wowote wa mwaka. Hatahivyo Hija kubwa hufanyika wakati maalumu katika mwezi wa Dhul Hija na hujumuisha amali maalumu kama vile kubakia usiku na mchana katika maeneo ya Arafah, Mina na Muzdalifa.

4066778

Kishikizo: iraq ، al kadhimi ، umrah ، saudi arabia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha