IQNA

Ibada ya Hija

Tume ya Hija Nigeria yasema nafasi zote zimejaa mwaka huu

23:09 - June 25, 2022
Habari ID: 3475424
TEHRAN (IQNA) – Tume ya Kitaifa ya Hija ya Nigeria (NAHCON) imelazimika kukataa maombi ya kuongeza nafasi zaidi kwa ajili ya Mahujaji mwaka huu ikisisitiza kuwa nafasi zote zimejaa.

NAHCON ilisema kwamba maombi hayo yalikataliwa kutoka kwa serikali za majimbo na mashirika mengine ya kibinafsi baada ya mgao ambao Saudia imeitengea Nigeria kumalizika.

Tamko hilo limekuja siku kadhaa  baada ya mamlaka ya Saudi kugawa nafasi 43,000 kwa ajili mahujaji kutoka Nigaria katika Ibada ya Hija mwaka huu wa 1443 Hijria Qamaria sawa na 2022 Miladia..

Mkurugenzi Msaidizi wa NAHCON wa Masuala ya Umma, Fatima Usara amesemaa mgao kwa nchi umekamilika na kwamba shirika hilo linatumai kuwa wasimamizi wote wa Hija watatumia nafasi walizotengewa..

Hata hivyo, alihakikishia bodi za Hajj za serikali na mashirika ya kibinafsi kwamba ikiwa Saudi Arabia itaheshimu ombi la nafasi za ziada, NAHCON iwafahamisha wahusika haraka.

Kulingana naye, hivi sasa bodi za mahujaji za majimbo yote na waendeshaji wa kibinafsi wanapaswa kuzingatia zaidi kuwatayarisha mahujaji wao ili wawasili kwa wakati kwa Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Hija mwaka huu.

Usara alisisitiza kwamba kazi kuu mbele ya NAHCON kimsingi ilikuwa kuwapelekea mahujaji wote waliosajiliwa hadi Ufalme kwa usalama kabla ya kufungwa kwa anga ya Saudia.

3479452

Kishikizo: nigeria hija saudia
captcha