IQNA

Waislamu wa Kanada

Waislamu Kanada wasaidia wasio na makao msimu wa baridi kali

23:32 - December 18, 2022
Habari ID: 3476267
TEHRAN (IQNA) - Wanachama wa Taasisi ya Misaada ya Kiislamu Kanada wametayarisha mamia ya vifurishi vya misaada maalumu ya majira ya baridi kali kwa ajili ya watu wasio na makazi wa Metro Vancouver siku ya Jumamosi.

Ufadhili huo unakuja wakati muhimu, kwani idara ya utabiri wa hali ya hewa Kanada imetabiri kuwa halijoto inaweza kushuka digrii tano hadi 10 chini ya wastani wa msimu katika siku zijazo.

"Tunajua, wakati baridi inapoanza inapoanza, ni watu wangapi wanaohitaji misaada," alisema Tahir Sattar, mshiriki wa jumuiya ya shirika hilo katika Kolombia ya Uingereza.

"Wanaishi mitaani katika hali ya kutisha, kwa hivyo tuko hapa tu kusaidia kuifanya hali iwe nyepesi kidogo na kuwapa kile wanachohitaji," akaongeza mfanyakazi wa kujitolea Soraya Elchehimi.

Kwa shirika, ambalo huhudumia jamii kimataifa na pia ndani ya nchi, ni kampeni ya sita ya kila mwaka ya kitaifa ya misimu ya joto kali na baridi kali.

Vifurishu vya misaada vinatolewa kwa mashirika ya mitaanikote katika jimbo ili kusambazwa.

Vifurushi hivyo vina glavu, soksi na blanketi; bidhaa za usafi kama sabuni, shampoo, pedi za usafi na manukato; pamoja na vipande maalumu vya kula venye virutibisho  na kadi za zawadi za $10 kwa ajili ya kununua bidhaa katika maduka ya mboga”.

Mbali na Metro Vancouver, vifurushi vya misaada pia vitasambazwa Kamloops, Prince George, Kelowna, Vancouver Island na Fraser Valley.

"Katika dini yetu, katika Uislamu, hisani ni moja ya vipengele vya msingi kwetu," alisema Elchehimi. "Ni wajibu kwa kila mmoja kusaidia jamii yetu."

3481728

captcha