IQNA

Kujipenyeza Wazayuni

Sheikh Issa Qassim asema ujenzi wa kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi mjini Manama ni jinai

17:24 - August 31, 2022
Habari ID: 3475711
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain amekosoa viikali uamuzi wa utawala wa Aal Khalifa wa kuanzisha kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi katika mji mkuu Manama na kueleza kwamba, hatua hiyo ni jinai na dhulma ya wazi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kiroho wa Mapinduzi ya Wananchi wa Bahrain amesisitiza katika taarifa yake kwamba, kujenga kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi katika mji wa Manama maana yake ni kubadilisha utambulisho wa kitaifa, Kiislamu na Kiarabu  na vile vile kitendo hicho kinapotosha historia ya nchi pamoja na nyaraka zake.

Ayatullah Issa Qassim ameongeza kuwa, kitendo hicho cha viongozi wa Manama kitawafungulia milango wavamizi wa Kizayuni na hivyo kupanga njama kwa urahisi na utawala wa Aal Khalifa.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain sambamba na kupinga vikali uamuzi huo ameeleza bayana kwamba, kufanya hivyo ni kutenda dhulma ya wazi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo pamoja na historia ya nchi yao.

Radiamali hiyo ya Sheikh Issa Qassim inafuatia kutangazwa mpango wa utawala wa Aal Khalifa wa kubadilisha kwa takribani asilimia 40 ya vitongoji vya kale katika mji wa Manama na kuvipa nembo na utambulisho wa Kiyahudi.

Tayari hivi sasa kuna ununuzi usiokoma wa majengo hayo ya kale tena kwa bei ya juu lengo likiwa ni kulibadilisha eneo hilo baadaye na kulifanya kuwa kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi.

Nchi nne za Kiarabu za Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco zilianzisha uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2020 kwa mashinikizo na upatanishi wa Marekani na bila ya kujali jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Hii ni katika hali ambayo Matokeo ya uchunguzi wa maoni yanaonesha kuwa, idadi kubwa ya watu wa Saudi Arabia, Imarati na Bahrain wanapinga suala la kuwepo uhusiano baina ya nchi hizo na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Utafiti huo uliofanyika miaka miwili baada ya nchi za Imarati na Bahrain kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni Israel, unaonyesha kuwa asilimia 71 ya Waimarati, 76 ya watu wa Bahrain na asilimia 75 ya Wasaudi Arabia wanapinga kuanzishwa uhusiano baina ya nchi hizo na utawala wa Kizayuni. 

Tangu ulipoanza ukandamizaji dhiidi ya vuguvugu la mapambano ya wananchi lililoanza mwaka Februari 14, 2011 hadi sasa, Bahrain imeendelea kushuhudia wimbi kubwa la malalamiko na upinzani wa umma unaotaka marekebisho ya kisiasa yafanyike nchini humo.  Katika kipindi chote hiki kunashuhudiwa makabiliano baina ya wanajeshi wa utawala wa Aal Khalifa na wananchi. Katika hali ambayo, utawala wa Aal Khalifa katika kipindi cha miaka 11 iliyopita, haujaheshimu haki yoyote ile ya wananchi wa nchi hiyo iwe ya kisiasa au ya kiraia, hivi sasa unataka kufanyike uchaguzi mpya wa Bunge.

4081786

captcha