IQNA

Hali ya Bahrain

Ripoti ya HRW kuhusu ukandamizaji wa wapinzani nchini Bahrain

7:45 - November 01, 2022
Habari ID: 3476019
TEHRAN (IQNA)- Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, utawala wa Bahrain unatumia sheria za kuwatenga kisiasa wapinzani.

Taarifa ya Human Rights Watch imeeleza pia kuwa, mbali na hatua hizo watawala wa Bahrain wanatumia mbinu zingine chafu za kuwafuta wapinzani katika ulingo wa kisiasa.

Sehemu nyingine ya ripoti hiyo ya Human Rights Watch imebajnisha kwamba, sharia za kuwatenga kisiasa wapinzani zilianza kutekelezwa nchini Bahrain kuanzia mwaka 2018 lengo likiwa ni kuwazuia wapinzani kuupata nyadhifa kama za Ubunge na nyadhifa nyingine katika idara za serikali.

Asasi hiyo imeutaka utawala wa Manama kufuta sheria hizo za kuwatenga kisiasa wapinzani sambamba na vitendo vya ukandamizaji vinavyofanya na vyombo vya usalama dhidi ya wanaharakati na wapinzani wa nchi hiyo.

Ikumbukwe kuwa, asasi za kutetea haki za binadamu zimekuwa zikitahadharisha mara kwa mara kuhusiana na ukandamizaji mkubwa unaofanywa nchini Bahrain na vyombo vya usalama dhidi ya raia na kutaka kukomesha vitendo hivyo.

Utawala wa kiimla nchini Bahrain umekuwa ukikandamiza wapinzani tangu ulipotumia mkono wa chuma mwaka 2011 kwa msaada wa utawala wa Saudi Arabia kupambana na maandamano na vuguvugu la umma la kupigania mageuzi ya kidemokrasia.

Mbali na adhabu za vifungo, utawala wa Aal Khalifa umewafutia uraia pia mamia ya Wabahrain katika kesi bandia zilizoendeshwa kwa umati na mahakama za utawala huo wa kifalme.

4095820

captcha