IQNA

Njama za Israel

Mtawala wa Bahrain amtimua waziri mwanamke aliyekataa kumpa mkono balozi wa Israel

18:48 - July 24, 2022
Habari ID: 3475534
TEHRAN (IQNA)- Mfalme wa Bahrain amemfuta waziri mwanamke wa nchi hiyo kwa kukataa kumpa mkono balozi wa utawala haramu wa Israel mjini Manama na kwa kupinga hatua ya kuanzisha ya uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu.

Hivi karibuni ilifanyika hafla katika makazi ya balozi wa Marekani nchini Bahrain ambapo Eitan Na'eh balozi wa utawala wa Israel nchini humo alihudhuria pia.

Wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Utamaduni na Turathi za Kale wa Bahrain Mai binti Muhammad Aal Khalifa alikataa kupeana mkono na balozi wa utawala wa Kizayuni na akaonyesha upinzani pia kwa hatua ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo bandia.

Kufuatia kujiri kwa tukio hilo, Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa Bahrain amechukua hatua ya kumuuzulu waziri huyo.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2020 utawala wa kifalme wa Bahrain ulisaini na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia baina ya pande mbili kwa upatanishi wa rais wa Marekani wakati huo Donald Trump; lakini tangu wakati huo hadi sasa upinzani wa wananchi wa Bahrain kwa hatua hiyo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu umekuwa kizuizi kikubwa kwa ustawishaji wa uhusiano kati ya Manama na Tel Aviv.

Bahrain ilitanguliwa na Muungano wa Falme za Kiarabu, UAE na kufuatiwa na Morocco na Sudan katika kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, hatua ambayo imekosolewa vikali ndani ya nchi zote hizo nne za Karabu na katika Ulimwengu wa Kiislamu, ikitafsiriwa kuwa ni sawa na kuyachoma jambia la mgongo na kuyasaliti malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.

Wananchi wa Bahrain huandamana mara kwa mara katika  mkuu Manama na miji mingine kupinga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Aidha tangu Februari mwaka 2011, wakati ulipoanza mwamko wa Kiisamu Asia Magharibi, Bahrain imekuwa uwanja wa maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa. Wananchi hao wanataka kuwepo uhuru, utekelezwe uadilifu, ukomeshwe ubaguzi na kuundwa serikali itakayochaguliwa na wananchi wenyewe.

3479803

captcha