IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israel walaaniwa kwa kuruhusu tamasha kwenye Msikiti wa Beersheba

22:12 - September 03, 2022
Habari ID: 3475727
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeulaani utawala haramu wa Israel kwa kuruhusu kuandaliwa matamasha katika Msikiti Mkuu wa Beersheba (Biʾr as-Sab).

Katika taarifa, Hamas ilisema: "Tunalaani kwa vikali utawala wa Israel kwa  kuruhusu matamasha na sherehe katika Msikiti Mkuu wa Beersheba."

Hamas ilisisitiza, "huu ni ukiukwaji wa wazi wa utakatifu wa msikiti," ikisema kwamba vitendo hivi "huwachukiza Waislamu wote duniani."

Harakati ya Wapalestina imeongeza kuwa: "Msikiti wa Beersheba na misikiti mingine yote ni mali ya wakfu wa Kiislamu, ambayo ni mali ya Waislamu ambao ni wakazi wa kipekee wa ardhi hii."

Ilisema: "Misikiti ya kihistoria inadumisha uhusiano kati ya ardhi hii na wakaazi wake halisi. Utawala wa utawala wa Israel na sera za kikoloni na uyahudishaji hazitafaulu kupotosha utambulisho wa Kipalestina ya kihistoria au kubadilisha ukweli wa kihistoria." Ikihitimisha taarifa yake, Hamas imewataka Wapalestina kukabiliana na sera hizo na kulinda ardhi zao na maeneo matakatifu kwa kila njia.

Kauli za Hamas zilikuja siku moja baada ya kuandaliwa kwa mfululizo wa matamasha na sherehe ndani ya ukumbi wa Msikiti Mkuu wa Beersheba.

3480330

captcha