IQNA

Jinai za Israel

Jeshi katili la Israel laua kijana wa Kipalestina huko Ukingo wa Magharibi

22:33 - September 15, 2022
Habari ID: 3475788
TEHRAN (IQNA) – Kijana wa Kipalestina aliuawa shahidi wakati wa uvamizi wa wanajeshi katili wa Israel karibu na mji wa Jenin katika sehemu ya kaskazini ya Ukingo wa Magharibi.

Jinai hiyo inakuja huku kukiwa na taharuki katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na utawala dhalimu wa Israel ambao jeshi la utawala huo limekuwa likiwakamata Wapalestina na kuwaua kiholela.

Kulingana na vyanzo vya ndani, kijana aliyeuawa shahidi alikuwa na umri wa miaka 17 na jina lake ni Uday Trad Salah. Alipigwa risasi na wanajeshi wa utawala haramu Israel kichwani wakati wa kuvamiwa mji wa Kafr Dan, magharibi mwa Jenin siku ya Alhamisi asubuhi.

Mvulana wa Kipalestina baadaye alifariki dunia kutokana na majeraha yake hospitalini.

Aidha, duru zimeongeza kuwa, Wapalestina wengine watatu walijeruhiwa wakati wa uvamizi huo, mmoja wao akiwa katika hali mbaya.

Kufuatia uvamizi huo, makabiliano yalizuka kati ya Wapalestina na wanajeshi wa Israel.

Taarifa zaidi zinasema wanajeshi katili wa Israel walivamia nyumba za wanaume wawili wa Kipalestina waliouawa siku ya Jumatano katika operesheni ya Jalama, na kuwahoji na kuwatia mbaroni watu wa familia zao.

Wapalestina Ahmad Ayman Abed, 23, Abdul Rahman Hani Abed, 22, waliuawa shahidi huku askari mmoja wa Israel akiangamia waliuawa wakati wa ufyatulianaji risasi katika Jalamah iliyoko karibu na kizuizi cha usalama kaskazini mwa Jenin.

Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) yenye makao yake makuu huko Gaza amesema kuwa, damu za Wapalestina wawili waliouawa shahidi hivi karibuni zitaimarisha zaidi mwamko wa Palestina na kupambana na utawala ghasibu wa Israel na kudhamini ushindi na ukombozi wa Palestina.

Wanajeshi wa Israel wanaendelea na operesheni zao za karibu kila siku za uvamizi na kamatakamata katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi ambapo Wapalestina huuawa na wengine hujurihwa katika oparesheni hizo.

Jinai hizo za jeshi la Israel zinaendelea huku walowezi wa Kizayuni nao pia wakiendesha vitendo vya ukatili dhidi ya Wapalestina.

Zaidi ya Wapalestina 70 wakiwemo watoto 37 wa Kipalestina wameuawa hadi sasa mwaka huu, wengi wao kutokana kupigwa risasi na askari wa utawala haramu wa Israel. Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa inasema jinai za Israel dhidi ya Wapalestina ni kinyume cha sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.

3480505

captcha