IQNA

Jinai za Israel

Wamarekani waandamana kulaani Google na Amazon kwa kushirikiana na Israel

20:35 - September 09, 2022
Habari ID: 3475755
TEHRAN (IQNA)- Wamarekani wamefanya maandamano katika baadhi ya miji ya nchi hiyo wakilaani jinai na hatua za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na hatua ya mashirika makubwa ya Google and Amazon kuunga mkono utawala huo.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unahesabiwa kuwa moja kati ya wavunjaji wakubwa wa haki za binadamu duniani. Utawala huo usiozingatia sheria na kanuni za kimataifa zinazohusiana na vita, tangu mwaka 2008 umeanzisha vita vinne dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kuua karibu watu 4,000, robo yao wakiwa watoto.

Waandamanaji katika baadhi ya miji ya Marekani ikiwemo New York na California, wakishirikiana na wafanyakazi wa Amazon na Google, wamepinga ukatili wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kuzitaka Amazon na Google zisitishe kutoa huduma kwa utawala huo wa Kizayuni.

Alhamisi ya jana, wanajeshi wa Kizayuni walimpiga risasi na kumuua raia mmoja wa Palestina katika lango la kijiji cha "Beitin", kilichoko kaskazini mashariki mwa Ramallah, karibu na kituo cha ukaguzi cha "Beit Il".

Siku ya Jumatano pia, wanajeshi hao wa Kizayuni walimuua kijana wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 21 kwa jina la "Younes Ghassan" kwa kumpiga risasi katika kambi ya al-Farah mkoani Tubas.

Hivi karibuni kundi la wafanyakazi wa Google walipinga mkataba wa dola bilioni 1.2 kati ya kampuni hiyo na Amazon na utawala wa Kizayuni.

4084346

captcha