IQNA

Mahmoud al-Toukhi, Qarii wa Misri ya ambaye anamuiga Sheikh Rafa'at

10:59 - June 11, 2020
Habari ID: 3472855
TEHRAN (IQNA) – Mahmoud al-Toukhi ni kati ya maqarii mashuhuri wa Misri wanaomuiga qarii mashuhuri Sheikh Mohammad Rafa'at.

Toukhi alizaliwa katika kijiji kimoja jimboni Qalyubiyya kaskazini mashariki mwa kaskazini mashariki mwa Misri na alianza kupenda kusoma Qur'ani akiwa bado mtoto.

Anasema baba yake alipelekea Madrassah ya Qur'ani akiwa mdogo na kwanza alihifadhi Qur'ani kabla ya kuanza kujifunza qiraa.

Toukhi anasema kwanza aliwaiga maqarii muhimu kama vile   Abdul Basit Abdul Samad, Mustafa Ismail, Mohamed Sidiq Minshawi na Mahmodu Ali al-Bana.

Sheikh Toukhi ametembea katika nchi nyingi duniani na anasema alitembelea madrassah za Qur'ani nchini Tanzania ambazo zinafunza qiraa yenye kuiga usomaji wa Wamisri.

Qiraa iliyopo hapa chini ni ile ambayo amemuiga Sheikh Mohammad Rafa'at.

3903538

captcha