IQNA

Mapambano ya Wapalestina

Ujumbe wa Hamas viongozi wa Kiislamu na Kikristo mjini Moscow

14:27 - September 15, 2022
Habari ID: 3475786
TEHRAN (IQNA) – Ujumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina ( Hamas ) umefanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Kiislamu na Kikristo katika mji mkuu wa Russia, Moscow.

Ujumbe huo, ukiongozwa na mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Ismail Haniyeh, uliwasili Moscow siku ya Jumamosi kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu ya kisiasa na maafisa wa Russia

Naibu mkuu wa Hamas, Saleh Arouri, na wajumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Mousa Abu Marzouq na Maher Salah, ni miongoni mwa maafisa wa Hamas walioshiriki aktika mazungumzo hayo.

Katika vikao hivyo, walikutana na Naibu Mufti wa Russia Sheikh Roshan Abbasov katika Msikiti Mkuu wa Moscow.

Pia walifanya mazungumzo na Sergey Zonarov, katibu wa uhusiano wa nje katika ofisi ya Kasisi Mkuu wa Moscow.

Wanachama waandamizi wa Hamas wameashiria juhudi za Hamas na wananchi wa Palestina za kuulinda mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) dhidi ya hujuma za Israel na majaribio ya utawala wa Kizayuni ya kutaka kuufanya mji huo kuwa wa Kiyahudi.

Pia wameangazia nafasi ya Waislamu wa Russia katika kutetea haki za Wapalestina na kupongeza kuwepo kwa amani kati ya imani tofauti nchini Urusi.

Sheikh Abasov alisisitiza uungaji mkono kutoka kwa Waislamu wa Russia kwa ajili ya Palestina, akisema wanafuatilia kwa karibu matukio ya al-Quds.

Katika mkutano mwingine, Zonarov alisisitiza kuwa Kasisi wa Moscow anapinga mipango ya Israel ya kubadilisha utambulisho wa kihistoria wa mji wa Quds

Ziara ya wajumbe wa Moscow ilikuja kufuatia mwaliko kutoka Moscow kujadili uhusiano wa pande zote na masuala mengine yanayohusiana na hali iliyopo Palestina.

 

4085662

captcha