IQNA

Russia na Uislamu

Moscow itaandaa Mkutano wa Mafunzo ya Kiislamu mnamo Februari 2023

14:05 - October 16, 2022
Habari ID: 3475937
TEHRAN (IQNA) – Kongamano la wanazuoni kuhusu masomo ya Kiislamu limepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Russia (Urusi) , Moscow mapema mwaka ujao.

Kongamano lililopewa anuani ya “Masomo ya Kiislamu; Ukweli, Mbinu na Ufafanuzi”, itaandaliwa na Taasisi ya Falsafa, Chuo cha Sayansi cha Urusi (Taasisi ya Falsafa ya RAS) kwa msaada wa Taasisi ya Utafiti wa Utamaduni wa Kiislamu ya Ibn Sina ya Russia.

Taasisi ya Utafiti ya Falsafa ya Iran pia itashirikiana katika kufanya tukio hilo la kielimu, ambalo limepangwa kufanyika Februari 2-3, 2023.

Mkutano huo unalenga kujadili masuala yanayohusiana na uwanja wa masomo ya Kiislamu katika zama za kisasa na njia zinazohitajika katika kusoma na kukuza ufahamu katika uwanja huu.

Kongamano hilo litafanyika katika lugha mbili za Kirusi na Kiajemi.

Wale walio tayari kushiriki katika mkutano huo wanaweza kuwasilisha muhtasari wa karatasi zao kwa anwani ya barua pepe islamphil@mail.com kabla ya tarehe 1 Novemba 2022.

Mada ambayo yatawasilishwa katika mkutano huo yatachapishwa katika jarida la Ishraq kuhusu falsafa ya Kiislamu.

4091980

captcha