IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Misri kuandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani mwezi Februari

18:39 - September 14, 2022
Habari ID: 3475783
TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly ameidhinisha mpango wa kuandaa Duru ya Sita Ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya nchi hiyo huko Port Said.

Tukio hilo la kimataifa la Qur'ani linalotarajiwa kuanza Februari 17 limepewa jina la marehemu Sheikh Nasreddin Tubar, mmoja wa maqari na wasomaji wa Ibtihal aliyefariki mwaka 1986.

Mashindano ya mchujo yanapangwa kufanyika mwezi ujao ili kuchagua wawakilishi wa Misri katika mashindano ya kimataifa. Haya yametangazwa na Adel al-Muslehi, afisa wa kamati ya maandalizi.

Uhifadhi wa Qur'ani nzima na usomaji wa Qur'ani kwa wanaume, kuhifadhi Qur'ani nzima kwa wanawake na swala na usomaji wa Tawasheeh ni kategoria za mashindano hayo, alisema. Muslehi aliongeza kuwa washiriki hawapaswi kuwa chini ya miaka 16 au zaidi ya miaka 30.

Kila mshindani anaweza kushiriki katika kitengo kimoja pekee, alisema, akibainisha kuwa wale ambao walishinda katika duru zilizopita hawawezi kushiriki shindano la mwaka huu.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Kurani ni za kawaida sana katika nchi ya Kiarabu na wengi wa qari wakuu wa ulimwengu wa Kiislamu hapo zamani na sasa wamekuwa Wamisri.

4085390

captcha