IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu

Waandaaji wataka mawazo mapya katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran

21:29 - December 11, 2022
Habari ID: 3476231
TEHRAN (IQNA) - Sekretarieti ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran imesema iko tayari kupokea mawazo na mapendekezo mapya kwa ajili ya kuandaa vyema tukio la kimataifa.

Sekretarieti hiyo, yenye mafungamano na Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu anayeshighulikia masuala ya Qur'ani Tukufu, imesema wale ambao wana mawazo na mapendekezo katika suala hilo wakiwemo wataalamu wanaweza kurejea tovuti ya maonesho hayo ya www.iqfa.ir ili kujisajili maoni yao.

Mapendekezo hayo yatatathminiwa na yale ambayo yanaonekana kuwa yanafaa na ambayo yatachangia uboreshaji wa maonyesho yatatekelezwa katika maonyesho yajayo.

Wale ambao wamependekeza mawazo bora pia watatunukiwa katika maonyesho hayo, sekretarieti iliendelea kusema.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza mafunzo ya Qur'ani Tukufu.

Aidha katika maonyesho hayo, huwasilishwa mafanikio ya hivi punde zaidi katika uga Qur'ani Tukufu nchini na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Mnamo 2020 maonyesho hayo yalisitishwa na mnamo 2021 yalifanyika kwa njia ya intaneti kutokana na janga la corona nchini.

Baada ya janga hilo kupungua, maonyesho hayo yalifanyika tena katika ukumbi mnamo Aprili 2022 kwa kauli mbiu ya "Quran, Kitabu cha Matumaini na Utulivu".

 4105988

captcha