IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu/ 38

Surah Saad: Kwa Nini Shetani Hakumtii Mungu?

22:24 - October 31, 2022
Habari ID: 3476014
TEHRAN (IQNA) – Imesemwa katika vyanzo vya kihistoria na kidini kwamba Shetani alikuwa mmoja wa watumishi maalum wa Mwenyezi Mungu waliokuwa wakimuabudu kwa muda mrefu.

Walakini, kwa sababu ya kutotii moja, alilaaniwa na kutengwa. Hii ni miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika Sura Saad ya Qur’ani Tukufu.

Saad ni sura ya 38 ya Qur’ani Tukufu yenye aya 88 na iko katika Juzuu 23 ya Qur’ani. Ilikuwa ni Sura ya 38 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina la Saad linatokana na herufi iliyotenganishwa ya Saad katika aya ya kwanza ya sura hii.

Maudhui ya Sura hii ni kuhusu Mtume Muhammad SAW alivyowalingania watu kufuata Tauhidi na Ikhlas (utakaso wa nia). Pia inahusu ukaidi wa makafiri, hadithi za baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, na maelezo ya hali itakavyokuwa Siku ya Kiyama kwa  wafanyao wema na waovu.

Pia inajumuisha mazungumzo kati ya Mwenyezi Mungu na Shetani na kufukuzwa na kulaaniwa kwa Shetani.

Mada kuu katika Sura hii ni mwaliko wa Mtukufu Mtume (SAW) kwenye tawhidi na Ikhlas pamoja na Kitabu ambacho Mwenyezi Mungu amemteremshia.

Vile vile inaangazia umuhimu na ulazima wa kuitafakari Qur'ani Tukufu na inataja baadhi ya matamshi ya makafiri kuhusu Kitabu hicho Kitukufu yaani Qur’ani Tukufu.

Hadithi za manabii tisa, akiwemo Dawud, Suleiman na Ayub, -Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yao-(AS), zimetajwa katika Surah Sad.

Pia sura hii inawataja Ibrahim (AS), Ismail (AS), Ishaq (AS), Yaqub (Yakub), Elisha (AS) na Dhu al-Kifl (AS) kuwa ni wajumbe na watumishi wateule wa Mungu.

Mwishoni mwa Sura, suala la kuumbwa kwa Adam na hadhi yake tukufu limetajwa. Malaika wanamsujudia kwa amri ya Mwenyizi Mungu lakini Shetani anamuasi Mwenyezi Mungu, akitaja uumbaji wake mkuu. Shetani anasema aliumbwa kwa moto lakini mwanadamu aliumbwa kwa udongo. Alikataa kumsujudia Adam na aliapa kujaribu kuwapoteza wanadamu mpaka Siku ya Kiyama.

Habari zinazohusiana
captcha