IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /40

Sharti la maombi kujibiwa

21:14 - November 12, 2022
1
Habari ID: 3476077
TEHRAN (IQNA) - Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 60 ya Sura Ghafir ya Qur'ani Tukufu kwamba, "Niombeni nami nitakuitikieni." Kwa hiyo sharti la maombi kujibiwa ni kwamba tumwite Mwenyezi Mungu.

Jina la sura ya 40 ya Qur'ani Tukufu ni Ghafir. Iko katika Juzuu ya 24 Juz ina aya 85. Sura Ghafir ni Makki na sura ya 60 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Ghafir maana yake ni "Mwenye kusamehe". Ni sifa ya Mwenyezi Mungu na inakuja katika Aya ya tatu ya Sura na hivyo kuipa sura hiyo jina lake.

Mada kuu ya Sura Ghafir ni kuonyesha kwamba majaribio ya makafiri kuharibu ukweli (Qur'ani) ambayo imetumwa kwao ni majaribio yaliyo batili na hayana maana. Mwenyezi Mungu anamkumbusha kila mtu hatima ya wale waliokadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu na aya za Mwenyezi Mungu na jinsi walivyopokea adhabu za Mwenyezi Mungu zilizokuwa zimeahidiwa.

Maudhui ya Sura yanaweza kugawanywa katika masuala kadhaa. Aya ya mwanzo inamzungumzia Mwenyezi Mungu  na sifa zake pamoja na baadhi ya majina yake mazuri. Kisha kuna maonyo kwa makafiri juu ya adhabu katika hapa duniani na kesho akhera. Baadaye, kuna marejeo ya kisa cha Musa (AS) na Firauni na kisa cha Muumini miongoni mwa masahaba wa Firauni.

Masuala mengine yaliyozungumziwa katika sura hii ni pamoja na dalili za Tauhidi, kukataa Shirki, kumlingania Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) awe na subira, na kuwakumbusha watu baadhi ya baraka za Mwenyezi Mungu. Pia kuna msisitizo wa kusafiri katika nchi mbalimbali ili kujifunza mafunzo kutokana na hatima za wale walioishi zamani.

Aya za 28 hadi 45 za Sura Ghafir zinamhusu muumini miongoni mwa masahaba wa Firauni. Alikuwa binamu yake Firauni na mtunza hazina wake. Alikuwa ameweka imani yake kwa Mungu kuwa siri hadi Musa (AS) alipoanza harakati yake. Baada ya kufichua imani yake, aliuawa na Firanu. Wakati mikono na vidole vyake vimepooza msalabani, alizungumza na watu na kuwaambia "Nifuateni." Ninakuongoza kwenye njia ya haki na ukamilifu."

Miongoni mwa mada nyingine zilizotajwa katika Sura Ghafir ni kujibu maombi. Mwenyezu Mungu anasema katika aya ya 60: "Niite nami nitakuitikia."

Katika tafsiri za Qur'ani imesemwa kuwa dua za makundi manne ya watu hazijibiwi: Mwenye kukaa nyumbani na kuomba riziki bila kufanya jitihada yoyote. Mwanaume anayemkasirikia mke wake na kuomba aondolewe. Mtu ambaye amepoteza mali zake kwa kuzifuja na sasa anamuomba Mwenyezi Mungu riziki. Na ambaye amempa mtu pesa kama mkopo bila ya kuwa na shahidi (na sasa anaomba kurejeshewa pesa zake).

Habari zinazohusiana
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
omary salim
0
0
nimependa haya mawaidha mungu akujaalie killa la kheri
captcha