IQNA

Uislamu na Mazingira

Uislamu unawafundisha wanadamu kuitunza sayari ya dunia

20:44 - November 24, 2022
Habari ID: 3476141
TEHRAN (IQNA) – Faiza Abbasi, mhadhiri wa vyuo vikuu nchini India ambaye mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Rasilimali Watu cha UGC, amesema Uislamu unafundisha ubinadamu na kutunza mazingira ya sayari ya dunia.

“Mtume Muhammad (SAW) alikuwa anapenda sana kupanda miti na alikuwa akiwahimiza maswahaba zake kufanya hivyo kwa kusema kuwa atakayepanda mti na kuutunza atapata ujira wake,” alisema Bi. Abbasi katika Kituo cha Khaliq Ahmad Nizami cha Mafunzo ya Qur’ani huko Aligarh, India.

Aliongeza kuwa changamoto za ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi zinaweza kupunguzwa kwa kuongeza ukanda wa kijani kibichi katika sayari ya dunia.

Waislamu wanaamini kwamba wanadamu lazima wawe walinzi wa sayari hii, na kwamba wanawajibika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa matendo yao, alisema, na kuongeza hii ni dhana yenye nguvu na imetumika katika Azimio la Kiislamu la Mabadiliko ya Tabianchi lenye lengo la kurekebisha sera ya mazingira katika nchi za Kiislamu.

Kwa upande wake, Profesa Abdul Rahim Qadwai (Mkurugenzi wa Heshima, Kituo cha Khaliq Ahmad Nizami) alisema: Harakati za kimazingira zenye msingi wa imani na theolojia ya Kiislamu zinapewa umuhimu kama mtazamo wa taaluma nyingi kote ulimwenguni.

Dk. Arshad Iqbal pia alizungumzia mimea iliyotajwa katika Quran Tukufu.

3481366

captcha