IQNA

Hujuma dhidi ya Uislamu

Maelfu waandamana Mali kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

11:35 - November 05, 2022
Habari ID: 3476038
TEHRAN (IQNA) - Makumi kwa maelfu ya watu walifanya maandamano siku ya Ijumaa katika mji mkuu wa Mali wa Bamako kushutumu kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Watu sita walikamatwa siku ya Alhamisi wakituhumiwa kushiriki katika kusambaza klipu ya video inayoonyesha mtu akitoa "matamshi ya dharau" na "vitendo vya matusi" dhidi ya Waislamu, Qur'ani Tukufu na Mtume Muhammad (SAW), ofisi ya mwendesha mashtaka wa Bamako ilisema.

Polisi walisema maandamano hayo, yaliyoitishwa na Baraza Kuu la Kiislamu la Mali (HCM), yalikusanya maelfu ya watu, ingawa waandaaji walikadiria idadi yao kuwa zaidi ya milioni moja.

Kauli mbiu zikiwemo "Hapana kwa maoni ya kukufuru" na "hakuna tena mashambulizi dhidi ya Uislamu na Mtume Muhammad SAW" zilionekana kwenye mabango ya waandamanaji.

Msomi wa Kiislamu, Sheikh Abdoulaye Fadiga amesema, "Kilichotokea hakiwezi kusameheka. Mwandishi wa maoni hayo ya kufuru lazima akamatwe na kuhukumiwa."

Haby Diallo, mwalimu katika shule ya kidini katika miaka yake ya 40, alisema anataka "mazungumzo baina ya dini. Kila mtu anapaswa kuheshimu dini ya mwenzake".

Watu hao sita waliwekwa kizuizini kabla ya kusikilizwa kwa kesi kwa kukataa kuwaambia maafisa wa usalama alipo mwenye kutoa matamshi hayo ya matushi mbapo mtu huyo .

Jambo hilo limezua ghasia nchini Mali, ambako karibu asilimia 95 ya wakazi ni Waislamu.

/3481126

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha