IQNA

Maulid ya Mtume Muhammad SAW

Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen: Wamagharibi waache kuvunjia heshima Matukufu ya Kiislamu

14:39 - October 09, 2022
Habari ID: 3475902
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa harakati ya muqawama ya Ansarullah ya Yemen alitoa wito kwa maafisa wa nchi za Magharibi kuacha kuivunjia heshima Qur'ani, Mtume Mtukufu (SAW) na matukufu mengine ya Kiislamu katika nchi hizo.

Katika hotuba ya Jumamosi ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), maarufu kama Miladun Nabii, kiongozi wa Ansarullah Sayyid Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi  alisisitiza watu wa Magharibi wanapaswa kukomesha uadui wao kwa maadili na kuacha kueneza ufisadi kati ya mataifa.

Makumi ya maelfu ya Wayemen walimiminika siku ya Jumamosi kwenye viwanja vya mji mkuu, Sana'a, na miji mingine kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume (SAW).

Washiriki waliwataka Waislamu kote ulimwenguni kusimama dhidi ya ubeberu wa Magharibi. Walishikilia mabango dhidi ya tawala za Marekani na Israel, ambazo zimeunga mkono muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi yao.

Kwingineko katika hotuba yake, Al Houthi aliutaka muungano unaoongozwa na Saudi Arabia kusitisha vita dhidi ya nchi yake, akisisitiza kuwa taifa la Yemen litaendelea kupinga uchokozi huo.

Ameutaka muungano wa vita kusitisha uchokozi, kuondoa mzingiro, na kukomesha kuikalia kwa mabavu Yemen.

Pia alitoa wito kwa "watu wetu wapendwa kuendelea kukabiliana na uvamizi maadamu unaendelea."

Aidha Al Houthi alisema Marekani na utawala wa Israel, pamoja na wafuasi wao, wanataka kufanya mataifa kuwa watumwa.

Alisema Marekani na Israel zimeelekeza juhudi zao zote katika kuwatoa watu kwenye nuru na kuwaingiza gizani.

Maandamano hayo yalifanyika wiki moja tu baada ya kumalizika kwa mapatano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa kati ya vuguvugu la Ansarullah na muungano huo. Makubaliano hayo yalianza kutekelezwa Aprili 2 kwa muda wa miezi miwili ya awali na yaliongezwa mara mbili hadi Oktoba 2.

Ufalme wa Saudia na washirika wake, haswa Umoja wa Falme za Kiarabu, wamekuwa wakiendesha vita dhidi ya Yemen tangu Machi 2015, wakijaribu, bila mafanikio, kuweka tena utawala wa kirafiki wa Saudi wa Abd Rabbuh Mansour Hadi.

Kampeni hiyo ya kijeshi ambayo imekuwa ikipata uungwaji mkono wa dhati wa silaha, vifaa na kisiasa kutoka Marekani, imeua mamia ya maelfu ya watu na kuigeuza Yemen nzima kuwa uwanja wa janga kubwa zaidi la kibinadamu duniani.

3480769

captcha