IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Marekani na waitifaki wanapinga mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu

18:00 - August 26, 2022
Habari ID: 3475682
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia katu haitalegeza msimamo mbele ya adui ili taifa hili liondolewe vikwazo vya kidhalimu vya Marekani.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Sala ya Ijumaa jijini Tehran na kueleza kwamba, timu ya Iran katika mazungumzo hayo ni aminifu na shujaa, hivyo haiwezi kufumbia macho haki za taifa hili la Kiislamu.

Ayatullah Khatami amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina mushkili na suala la kufanya mazungumzo, lakini jambo la msingi ni kuwa Marekani na waitifaki wake tatizo lao ni mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na siyo kadhia ya mradi wa nyuklia wa taifa hili kama wanavyodai.

Ameongza kuwa, Marekani na waitifaki wake wanapinga na hawataki kuona kunakuweko Iran yenye mshikamano na ambayo ndio nguvu kubwa kabisa ya kielimu katika eneo la Asia Magharibi.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran amebainisha kuwa, ni lazima kuwa na nguvu mbele ya adui na kusimama kidete na kwamba, wananchi wa Iran si wenye kuchoka na wamesimama imara wakiwa na ukakamavu kamili kwa ajili ya kutetea mapinduzi yao ya Kiislamu.

Ayatllah Khatami ameashiria pia kuanza maadhimisho ya wiki ya serikali hapa Iran na kusema kuwa, serikali ya awamu ya 13 inayoongowa na Sayyid Ibrahim Raisi ina mawasiliano na maingiliano na wananchi, na miongoni mwa sifa muhimu za serikali hii ni kutekeleza kivitendo ahadi ilizotoa.

 

4080839

captcha