IQNA

Kombe la Dunia Qatar

Watumiaji wa Twitter wavutiwa na sauti ya adhana wakati wa mazoezi ya Timu ya England nchini Qatar + Video

16:33 - November 19, 2022
Habari ID: 3476114
TEHRAN (IQNA) – Watumiaji wengi wa Twitter walipendezwa na sauti nzuri ya Adhana baada ya klipu iliyorushwa na mwandishi mkuu wa kandanda wa Times Henry Winter iliyoonyesha mazoezi ya timu ya England wakati wa Adhana kusambaa mitandaoni.

Adhana ni wito wa Kiislamu wa kutangaza kwamba umefika wakati wa Sala maalum ya faradhi ya kila siku.

Klipu hiyo  lilisambaa 'kupendwa' mara 7000 na kutumwa tena mara 1000 baada ya muda mfupi. Wafuasi wengi wa Winter walishiriki kuvutiwa na sauti nzuri ya Adhana.

Inafurahisha, Henry Winter ni kaka wa Skeikh Abdal Hakim Murad, mkuu wa Chuo cha Waislamu cha Cambridge.

 

 

Abdal Hakim, ambaye zamani kabla ya kusilimu alikuwa Timothy John Winter, ni msomi wa Kiingereza, mwanatheolojia na mwanazuoni wa Kiislamu ambaye alisilimu mnamo 1979.

Saa chache kabla ya kuzinduliwa kwa Kombe la Dunia 2022, Qatar ilizindua mipango kadhaa ya kutambulisha Uislamu kwa wageni wakati wa mashindano hayo ya soka ya kimataifa.

Kwa mfano, katika katika vyumba vya wageni vya hoteli za Qatar kuna QR Code ambayo inatoa maelezo kwa wageni kuhusu Uislamu na utamaduni wa Qatar katika lugha zote.

Qatar pia imeweka  maandishi makubwa  kote nchini humo yenye hadith za Mtume Muhammad (SAW) ili kutambulisha Uislamu kwa mashabiki wanaokuja wa Kombe la Dunia.

Kwingineko, mashabiki waliosafiri kuelekea Qatar kwa ajili ya Kutazama Kombe la Dunia la 2022, hawataruhusiwa kunywa pombe viwanjani.

 

Kishikizo: adhana ، kombe la dunia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha