IQNA

Kombe la Dunia la Qatar

Mashabiki wa Kombe la Dunia washiriki katika Sala ya Ijumaa mjini Doha + Video

21:04 - November 26, 2022
Habari ID: 3476152
TEHRAN (IQNA) – Mashabiki wa soka wa Waislamu ndani na nchi na kutoka mataifa mengine duniani walihudhuria Sala ya Ijumaa mjini Doha, Qatar huku Kombe la Dunia la kwanza katika nchi ya Kiislamu likiendelea.

Ilipofika saa sita mchana, waadhini kote nchini Qatar walitamka walisikika wakiwaita Waislamu wakiwemo wachezaji wa soka, mashabiki, maafisa wa soka na wote kwa ujumla kwenye sala ya Ijumaa ya kwanza ya Kombe la Dunia la Kwanza kufanyika katika nchi ya Kiislamu.

Katika Msikiti wa Ibrahim Al Khalil katika eneo la Doha West Bay wenye mnara mrefu na milango ya mbao iliyochongwa, Waislamu walikusanyika kwa ajili ya Sala ya jamaa ya Ijumaa.

Miongoni mwa waumini walikuwa mashabiki kutoka Tunisia, Oman na India, afisa wa Fifa aliyevalia sare, watoto waliovalia sare za soka za Ufaransa na mamia ya wanaume na wanawake kutoka hoteli zilizo karibu na viwanja vya minara.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa kandanda, mashabiki wa Kiislamu wanasema Kombe la Dunia la Qatar limefanya wahisi wako nyumbani kwa njia ambayo haijawahi kushuhudiwa kwani kuna vyumba vya sala katika viwanja vya mpira, kuna vyakula 'Halal' na hakuna mashabiki wenye kunywa pombe dani ya viwanja  kufuatia marufuku ya pombe uwanjani.

"Nimekuja katika nchi ya Kiislamu na ninahudhuria Sala ya Ijumaa...Hili ndilo linalonifurahisha katika mashindano haya," alisema Yousef al Idbari, shabiki kutoka Morocco.

Kama waumini wengine wote, al Idbari, alivua viatu vyake na kuingia ndani ya jumba kuu la sala ndani  msikiti.

Uislamu umeonekana wazi wazi katika wiki nzima ya kwanza ya mashindano hayo kutokana na hatua inayoendelea kupongezwa ya kufungua mashindano ya qiraa ya Qur'ani Tukufu pamoja na Hadithi za Mtume Muhammad (SAW) zilizoandikwa katika kuta za maeneo mbali mbali Doha.

Mashabiki wa Kiislamu wanafurahia Kombe la Dunia mwaka huu ambalo linakidhi mahitaji yao.

Ridwaan Goolam Hoosen, shabiki wa soka wa Afrika Kusini mwenye shauku, amezoea kuondoka uwanjani kutafuta nafasi ya Sala, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini.

3481407

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha