IQNA

Kombe la Dunia la Qatar

Mashabiki wa Tunisia wanaunga mkono Palestina wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia la 2022

17:56 - November 27, 2022
Habari ID: 3476156
TEHRAN (IQNA) – Mashabiki wa Tunisia waliinua bendera ya 'Palestine Huru' dakika ya 48 dhidi ya Australia kumkumbuka Tukio la Nakba.

Mashabiki wa Tunisia walipeperusha bendera ya "Palestine Huru" katika dakika ya 48 ya mechi yao ya Kombe la Dunia la Qatar dhidi ya Australia siku ya Jumamosi, wakimaanisha kile kinachojulikana na Waarabu kama Nakba ya 1948 wakati mamia ya maelfu ya Wapalestina walipotimuliwa kutoka nchi yao na wanamgambo wa Kizayuni na baada ya hapo ukanduwa utawala bandia na haramu wa Israel.

Licha ya Palestina kutofuzu kwa michuano hiyo inayofanyika Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) kwa mara ya kwanza, lakini bendera yake ya taifa hilo imekuwa alama inayotambulika kila mahali katika kipindi chote cha mashindano hayo.

Mashabiki wa kandanda wa Tunisia na Waarabu wengine wamejitolea kuonyesha bendera za Palestina na kuvaa shela za Wapalestina mabegani mwao.

Hisia chanya na mshikamano wa mashabiki wa soko na taifa la  Palestina ni mkubwa kiasi kwamba katika video moja ya mtandaoni, shabiki wa Misri, akitabasamu, anaegemea kwenye kamera ya mtangazaji wa utawala wa Israel na kumpa ujumbe sahali usemao: "Viva Palestine."

Machapisho ya mitandao ya kijamii katika siku za hivi majuzi yanaonyesha mashabiki ambao, baada ya kutambua kuwa wanahojiwa na vyombo vya habari vya Israel, wanajizuia kuzungumza au kutoa wito wa ukombozi wa Palestina.

Ingawa Qatar na Israel hazina uhusiano rasmi, kwa mara ya kwanza, kuna safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tel Aviv na Doha, huku mashabiki na maafisa wa kidiplomasia wa Israel wakiruhusiwa nchini humo kwa mara ya kwanza.

Kabla ya michuano ya Kombe la Dunia mjini Doha, mamia ya mashabiki walikusanyika na kupeperusha bendera ya Palestina, huku ripoti zikisema kuwa ilikuwa ni sehemu ya hafla iliyoandaliwa na kundi la Qatar Youth Against Normalization ambalo linapinga uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel..

Siku ya Nakba kwa Wapalestina ni siku katika mwezi Mei 1948, ambapo zaidi ya robo tatu ya eneo la kihistoria na la asili la ardhi ya Palestina lilipovamiwa na kukaliwa kwa mabavu, Wapalestina 531 walipouliwa; na kufukuzwa na kugeuzwa wakimbizi karibu asilimia 85 ya idadi ya watu wa Palestina waliolazimika kukimbilia nchi jirani ikiwemo Jordan, Syria, Lebanon na baadhi ya nchi nyingine za nje ya Ukanda wa Asia Magharibi, kama inavyoeleza ripoti ya idara kuu ya takwimu ya Palestina.

3481422

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha