IQNA

Jinai za Israel

Jeshi katili la Israel laua shahidi Wapalestina watatu huko Jenin

18:56 - December 08, 2022
Habari ID: 3476216
TEHRAN (IQNA)-Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limewaua shahidi vijana watatu wa Kipalestina katika mji wa Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Vijana hao wa Kipalestina wameuawa shahidi mapema leo baada ya wanajeshi makatili wa Israel kushambulia kambi ya wakimbizi huko Jenin.

Habari zaidi zinasema kuwa, Wapalestina hao wameuawa shahidi katika makabiliano na wanajeshi hao wa Israel, ambao pia wamejeruhi Wapalestina wengine kadhaa.

Duru za hospitali katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu zimewataja wahanga hao waliouawa kikatili kwa risasi za Wazayuni kuwa ni Tariq Aldamj, Siddiqui Zakarneh na Atta Shilbi.

Habari zaidi zinasema kuwa, makumi ya watu wamejeruhiwa baada ya wanajeshi makatili wa Israel kuumiminia risasi mkusanyiko wa Wapalestina nje ya kituo cha matibabu karibu na kambi hiyo ya wakimbizi. Askari hao wa Kizayuni wameharibu kikamilifu kwa risasi ambulensi ya kituo hicho cha afya mjini Jenin.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Wapalestina zaidi ya 216 wameuawa shahidi na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 hadi sasa, wakiwemo 164 katika Ukingo wa Magharibi na 64 katika Ukanda wa Gaza.

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika miezi ya hivi karibuni limelazimika kusitisha mara kadhaa mashambulizi yake dhidi ya mji wa Jenin, likihofia majibu ya makundi ya wanamapambano wa Kipalestina.

Kishikizo: palestina jenin wazayuni
captcha