IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wavamia Msikiti wa Al-Aqsa chini ya ulinzi wa Jeshi la Israel

22:31 - November 27, 2022
Habari ID: 3476158
TEHRAN (IQNA) - Kundi la walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali walivamia Msikiti wa Al-Aqsa huko mjini Al Quds (Jerusalem) wakiwa wametekeleza hujuma hiyo Jumapili asubuhi.

Walowezi hao waliingia msikitini chini ya ulinzi mkali wa polisi wa utawala vamizi na wa kikoloni wa Israel.

Polisi wa utawala ghasibu wa Israel waliendelea kuweka vikwazo vya kuwazuia Waislamu Wapalestina kuingia ndani ya msikiti huo.

Wakati huo huo, wito umetolewa kwa Wapalestina wenyeji wa mji  Al Quds kujitokeza kwa wingi katika Msikiti wa Al-Aqsa ili kukabiliana na uvamizi wa walowezi  wa Kizayuni  ambaoo  wanatekeleza mpango wa Israel  wa Kuyahudisha  mji wa Al Quds na Msikiti wa Al Aqsa mjini humo.

Kila siku, isipokuwa siku ya Ijumaa na Jumamosi, Al-Aqsa inakumbwa na mfululizo wa uvamizi wa walowezi, nyakati za asubuhi na jioni. Uvamizi huo ni sehemu ya majaribio ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutekeleza njama mpya katika Msikiti wa Al Aqsa kwa kuongeza masaa ambayo Wazayuni wanaruhusiwa kuwa ndani ya msikiti huo yaani kuuhujumu.

Mpango huu ni katika fremu ya utawala wa Kizayuni kuugawa Msikiti wa Al Aqsa kwa mujibu wa kile kinachotajwa kuwa ‘mahala na wakati’

3481420

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha