IQNA

Mwaka wa 44 wa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

IQNA yaandaa warsha ya intaneti kujadili Mapinduzi ya Kiislamu

21:23 - February 07, 2023
Habari ID: 3476527
TEHRAN (IQNA) – Warsha ya kimataifa inatazamiwa kufanyika siku ya Jumatano kwa njia ya intaneti kwa lengo la kujadili Mapinduzi ya Kiislamu.

Warsha hiyo imeandaliwa na shirika la habari la IQNA na mada kuu itakuwa "Mazungumzo Kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu Katika Mchakato wa Mageuko." Warsha ambayo inafanyika kwa njia ya intaneti (Webinar) Februari 8 itaanza saa Tatu na Nusu kwa Majira ya GMT.

Wazungumzaji wa hafla hiyo ni mshauri wa rais wa Iran katika masuala ya vyuo vya Kiislamu au Hauza Hujjatul Islam Mohammad Haj-Abolghasemi, naibu waziri wa ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Seyyed Mahdi Farahi, msomi wa Lebanon na mjumbe wa baraza la kisiasa la Hezbollah Bilal Al-Laqis, na Bi Zeenat Ibrahim, mke wa Sheikh Ibrahim Zakzaki, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Unaweza kufuatilia Webinar hiyo kwa kubonyeza  Aparat na Roytab.

Kikao hicho kimeandaliwa kwa mnasaba wa mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Int’l Webinar to Discuss Islamic Revolution Discourse

4120185

captcha