IQNA

Uislamu na Ukristo

Papa Francis akisikiliza qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Qari wa Iraq (+Video)

18:41 - December 19, 2022
Habari ID: 3476271
TEHRAN (IQNA) – Papa Francis, katika ziara ya kwanza ya kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, alisafiri hadi Iraq mwezi Machi mwaka jana.

TEHRAN (IQNA) – Papa Francis, katika ziara ya kwanza ya kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, alisafiri hadi Iraq mwezi Machi mwaka jana.

Katika safari hiyo ya kihistoria, alikutana na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia Ayatullah Seyed Ali al-Sistani katika mji mtakatifu wa Najaf.

Moja ya sehemu alizotembelea wakati wa ziara hiyo nchini Iraq ni mji wa kale wa Ur, mji wa Kisumeria ambao ulianzishwa miaka 6,000 iliyopita na inaaminika kuwa ndiko alikozaliwa Nabii Ibrahim (AS).

Katika ziara hiyo, Papa Francis alisoma dua ya pamoja ya dini za Ibrahimu (Uislamu, Ukristo na Uyahudi) iliyopewa jina la "Sala ya Watoto wa Ibrahimu". Baada ya hapo alisikiliza usomaji wa Qur'an Tukufu wa Qari maarufu wa Iraq Osama al-Karbalayi.

Ufuatao ni usomaji wa Al-Karbalayi wa aya za 40 na 41 za Sura Ibrahim za Qur'an Tukufu siku hiyo:

"Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu.  Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu."

4107798

captcha