IQNA

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Damu safi ya mashahidi inkabiliana na ujahilia unaoenezwa na maadui

21:53 - March 14, 2023
Habari ID: 3476704
TEHRAN(IQNA)-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Leo hii ambapo maadui wanataka kuenenza fikra na mienendo ya ujahilia mamboleo katika jami, ni damu safi ya mashahidi ndiyo inayoondoa na kukabiliana na ujahilia huo.

Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Shahidi, iliyofanyika kwa kuhudhuriwa na familia za mashahidi katika Msikiti wa Salman Farsi mjini Tehran. Ameongeza kuwa: "Siku ya Shahidi ina umuhimu mkubwa, kwa sababu kwa mara nyingine tena inakumbusha jina, njia na lengo la mashahidi.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja usalama, umoja, mshikamano na adhama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni matokeo ya damu safi ya mashahidi waliouawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kuongeza kuwa: “Tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, maadui walianzisha mbinu za kueneza hali ya kukata tamaa baina ya wananchi kupitia njia ya kufanya njama, kuibua fitina na mizozo ya aina mbalimbali, lakini mashahidi walitufunza, si kwa maneno bali kwa vitendo, kwamba tunaweza kushinda vizingiti hivyo vyote kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu.” 

Rais Ebrahim Raisi ameyataja machafuko ya hivi karibuni katika baadhi ya miji ya Iran kuwa ni vita mseto vya adui katika sekta ya vyombo vya habari, kiuchumi na kifikra kwa lengo la kukwamisha maendeleo ya taifa la Iran. Amesema kuwa: Uzoefu wa miaka 44 wa Jamhuri ya Kiislamu umeonyesha kwamba, maadui wamegonga mwamba mbele ya taifa la Iran, na hawatafika popote baada ya hapa, kwa sababu, licha ya mashinikizo na vikwazo, taifa la Iran limepata mafanikio makubwa na ya kujivunia katika nyanja mbalimbali.

4128091

captcha