IQNA

Jinai za Israel

Indhari kuhusu njama ya Israel ya kugeuza eneo la Kiislamu la Bab Al-Rahma kuwa Sinagogi

17:28 - April 26, 2023
Habari ID: 3476917
TEHRAN (IQNA) - Kundi la kutetea haki za binadamu limeonya kuhusu njama ya utawala ghasibu wa Israel kugeuza Jumba la Sala la Bab Al-Rahma katika Msikiti wa Al-Aqsa kuwa sinagogi.

Kamati ya Kiislamu-Kikristo inayounga mkono Quds (Jerusalem) na Maeneo yake Matakatifu imeonya kwamba utawala haramu wa Israel unapanga kugeuza Jumba la Sala la Bab Al-Rahma kuwa sinagogi la Kiyahudi.

Bab Al-Rahma ni sehemu ya Kiwanja cha Msikiti wa Al-Aqsa na eneo hilo limekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel tangu mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika taarifa yake, kamati hiyo ilionya juu ya mpango uliopangwa tayari wa Israel wa kuuyahudisha Msikiti wa Al-Aqsa, ikisema kwamba "kutenganisha Msikiti wa Bab Al-Rahma na eneo lote la Msikiti wa Al-Aqsa na kuugeuza kuwa sinagogi la Kiyahudi ni sehemu ya mpango huo."

Kamati hiyo ilitoa wito kwa Wapalestina wote "kukabiliana na jaribio la Israel la kuufunga Msikiti wa Bab Al-Rahma". Ili kukabiliana na jama hiyo, Waislamu Wapalestine wametakiwa kukarabati na kuanza tena kusali ndani ya Bab Al-Rahma."

Katika taarifa hiyo, kamati hiyo ilisisitiza kuwa "jaribio lolote la kubadilisha hali ilivyo sasa katika Bab Al Rahma litakuwa na matokeo hatari ambayo uvamizi wa Israel utalaumiwa."

Siku ya Jumatatu, wanajeshi wa Israel walivamia Bab Al-Rahma na kukata vifaa vya umeme kwa mara ya pili ndani ya siku tano.

Waliwaweka kizuizini wanaume wawili wa Kipalestina na mwanamke wa Kituruki waliokuwa wakisali ndani, na kuwataka walinzi wa Msikiti wa Al-Aqsa kutokarabati umeme wa eneo hilo. Mwanamke huyo wa Kituruki aliachiliwa siku moja baadaye.

3483337

captcha