IQNA

Jinai za Israel

Wanajeshi wa Israel wazuia Waislamu kusali Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa

20:26 - February 23, 2024
Habari ID: 3478401
IQNA - Vikosi vya Israel vimewashambulia waumini karibu na lango la Asbat, lango kuu la kuingia Msikiti wa Al-Aqswa katika mji Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, wakiwazuia na kuwapiga walipokuwa wakijaribu kuingia msikitini humo kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.

Pia waliwashambulia watu katika kitongoji cha karibu cha Wadi al-Joz, ambapo walimkamata mtoto, Shirika la Habari la WAFA la Palestina liliripoti.

Walioshuhudia wanasema askari katili wa Israel waliwasaili na kuwapekua raia wa Palestina, wakiwazuia kutoka Mji Mkongwe wa Al Quds na Msikiti wa Al-Aqsa. Waliweka vizuizi vya polisi na kuwadhulumu baadhi ya watu, haswa kwenye lango la Asbat. Pia walimshikilia mtoto baada ya kumshambulia karibu na makaburi ya Yeusefiya karibu nayo.

Licha ya vizuizi vya wanajeshi katili wa Israel kwenye lango la msikiti huo, idadi ndogo ya waumini waliweza kuswali hapo siku ya Ijumaa, wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara na dhuluma. Hii ilikuwa ni Ijumaa ya ishirini mfululizo na matukio kama haya.

Wakfu wa Kiislamu umesema ni waumini wachache tu wanaoweza kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa kwa sababu ya vikwazo vya utawala haramu wa Israel na vizuizi vya polisi katika Mji Mkongwe wa al-Quds.

Vikosi vya utawala wa Israel vilikuwa vimekaa kwenye lango la Mji Mkongwe, ukiwemo Msikiti wa Al-Aqsa, tangu mapema asubuhi, na kushadidisha  hujuma dhidi ya Waislamu katika eneo hilo takatifu. Pia walivamia jumba la Qubbat aṣ-Sakhra ili kuzuia waumini wasifike eneo hilo ambalo ni sehemu ya uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa.

3487308

Habari zinazohusiana
captcha