IQNA

Kadhia ya Palestina

Idadi kubwa ya waumini wajitokeza Sala ya Ijumaa Msikiti wa Al Aqsa

21:10 - September 02, 2023
Habari ID: 3477538
Al QUDS (IQNA) - Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Ijumaa ya jana iliyosaliwa kwenye Msikiti wa Al-Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) licha ya kuwekewa vizuizi na kukabiliwa na hatua kali za kiusalama zilizochukuliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mji huo unaoukalia kwa mabavu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina, makumi ya maelfu ya waumini wa Kipalestina walisali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa hapo jana katika mazingira ya kuogofya ya ulinzi mkali na msharti magumu yaliyowekwa na utawala ghasibu wa Israel kwa ajili ya kuingia katika mji wa Baitul Muqaddas.

Sala ya Ijumaa ya jana, sawa na ya wiki iliyopita ilisaliwa katika hali ambayo mamlaka za utawala dhalimu wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds tukufu ziliweka vizuizi vikali vya kuwazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa.

Vikosi vya jeshi la utawala wa Kizayuni vilijaribu kuwazuia Wapalestina kuingia katika msikiti huo wakitokea Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa kusambaa katika maeneo tofauti ya mji huo na kuweka vituo vya upekuzi kuzunguka mji wa Baitul Muqaddas au Al Quds, sambamba na kuchukua hatua za kuwafanyia upekuzi mkali raia wa Palestina.

Uvamizi na uvunjiaji heshima wa mara kwa mara wa Wazayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa unafanyika huku taasisi za kimataifa na za kutetea haki za binadamu zikiwa zinaendelea kulinyamazia kimya suala hilo.

4166298

Habari zinazohusiana
captcha