IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu katika jiji lenye watu wengi zaidi Brazil

19:13 - April 30, 2023
Habari ID: 3476937
TEHRAN (IQNA) – Sao Paulo, jiji lenye watu wengi zaidi nchini Brazili, ni mwenyeji wa maonyesho ya Qur’ani Tukufu yatakayoandelea kwa wiki moja.

Maonyesho hayo yanaanza Jumatatu, Mei 1, na yataendelea hadi Mei 8 na yameandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia.

Sidney Romero, mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazili, na maafisa kadhaa jiji hilo watashiriki katika hafla ya uzinduzi huo.

Pia uzinduzi wa maonyesho hayo utahudhuriwa na  wahitimu Wabrazili wa vyuo vikuu vya Saudi na afisa kutoka Kituo cha Kiislamu cha Dawah huko Amerika Kusini.

Maonyesho hayo yataonyesha nakala za kale za Qur'ani Tukufu na machapisho ya Kituo cha Uchapishaji Qur'ani Tukufu cha Mfalme Fahd.

Wageni pia watatunukiwa tafsiri za Qur'ani Tukufu katika lugha tofauti.

Kituo cha Uchapishaji Qur'ani Tukufu cha Mfalme Fahd, ambao kiko katika mji mtakatifu wa Madina, kimechapisha tafsiri za Qur'ani katika zaidi ya lugha 40 tofauti.

Kituo hicho aidha huchapisha nakala takribani milioni 10 za Qur'ain Tukufu kila mwaka.

Brazil ni nchi kubwa katika Amerika ya Kusini. Uislamu unafuatwa na zaidi ya Wabrazili 200,000—na hivyo ni jumuiya kubwa zaidi ya Waislamu katika Amerika Kusini.

Wengi wa Waislamu wa nchi hiyo wana asili ya Waarabu, na idadi ndogo lakini inayoongezeka ni ya Wabarazil waliosilimu.  Jumuiya ya Waislamu wa Brazil inajumuisha Waislamu wa Sunni na Shia.

4137329

captcha