IQNA

Msikiti wahujumuwa Ponta Grossa, Brazil

15:29 - November 29, 2021
Habari ID: 3474615
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Imam Ali huko Ponta Grossa nchini Brazil umehujumiwa Ijumaa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu, wametangaza wasimamizi wa msikiti huo.

Katika taarifa kupitia Instagram, wasimamizi wa Msikiti wa Imam Ali AS wamesema hujuma hiyo imejiri Ijumaa usiku ambapo watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wameteketeza moto Qur'ani Tukufu huku wakiharibu kuta za msikiti.

"Jinai hii haijaulengatu Uislamu, bali ni hujuma dhidi ya dini zote kwani hujuma hiyo imelenga maneno na nyumba ya Mwenyezi Mungu," imesema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Arede, waliotekeleza jinai hiyo waliingia msikitni kwa kuvunja mlango wa pembeni. Katika hujuma hiyo pia waliteketeza moto maandishi ya Kiislamu yaliyokuwa ukutani na tasbihi zilizokuwa msikitini hapo. Hakuna chochote kilichoibiwa katika hujuma hiyo na hivyo inaaminika kuwa wahusika walikuwa ni watu wenye misimamo mikali kwa lengo la kuumiza hisia za Waislamu.

4016970

Kishikizo: msikiti ، brazil ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha