IQNA

Qurani Tukufu

Ndugu wawili Misri wenye ulemavu wa macho wapata umaarufhu katika usomaji Ibtihal

15:39 - May 08, 2023
Habari ID: 3476977
TEHRAN (IQNA) – Mohammed na Iman ni kaka na dada wa Kimisri ambao umahiri wao katika usomaji wa Ibtihal umewapatia umaarufu nchini humo.

Kulingana na tovuti ya youm7, Iman Wael Ahmed Qarib yuko katika darasa la 9 na kakake Mohammed yuko darasa la 7.

Wanaishi Dirb an-Najm, mji ulioko katika Jimbo la Sharqia nchini Misri.

Ndugu hao wenye ulemavu wa macho wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, walianza kujifunza Kitabu Kitakatifu kwa moyo wakiwa na umri mdogo.

Iman alianza kuhifadhi saa sita na akahifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu  katika muda wa miaka miwili.

Pia alijifunza sheria za Tajweed na mitindo kumi ya usomaji, na hivyo kupokea kibali cha usomaji wa Kurani akiwa na miaka 12.

Muhammad alihifadhi Quran katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia akiwa na umri wa miaka 6.

Ndugu hao wawili wameshindana katika mashindano tofauti ya Qur'ani na kushinda baadhi yao.

Wanapenda kusikiliza visomo vya Qur'ani vya Abdul Basit Abdul Samad, Mohammed Rif’at, Mahmoud al-Khisht, Ahmed Nuaina na Abdul Fattah al-Taruti.

Ndugu wanajulikana zaidi kwa talanta yao katika usomaji wa Ibtihal.

Ibtihal ni kisomo cha dua na qasida, zikiwemo zile za kumsifu Mtukufu Mtume (SAW).

captcha