IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Port Said Misri yaanza

13:47 - February 18, 2023
Habari ID: 3476578
TEHRAN (IQNA) – Toleo la sita la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Port Said yameanza Ijumaa katika mji huo wa bandarini Misri.

Jumla ya washiriki 65 kutoka nchi 41 watachuana katika kategoria tofauti ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani Tukufu, Dua na Ibtihal.

Mashindano ya mwaka huu yamepewa jina la marehemu Sheikh Nasreddin Tubar, qari mashuhuri wa Qur’ani Tukufu ambayo pia alipata ummarufu kwa usomaji wa Ibtihal aliyefariki mwaka 1986.

Sherehe za ufunguzi zilifanyika kwa mahudhurio ya viongozi wa Misri akiwemo Waziri wa Wakfu Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa.

Sherehe ilianza kwa usomaji wa aya za Quran tukufu na Ibtihal. Idadi ya wasomi wa kidini na familia zao pia walitunukiwa katika hafla hiyo.

Mbali na Misri, wawakilishi kutoka UAE, Tunisia, Algeria, Sudan, Palestine, Jordan, Nigeria, Kenya, Canada, Lebanon, Morocco, Amerika, Yemen, Ethiopia, Indonesia, Uganda, Pakistan, Chad na India pia wanashiriki mashindano ya mwaka huu.

4122790

captcha