IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wapalestina wa Al-Quds washiriki mashindano ya 'Familia ya Qur'ani'

14:45 - November 17, 2022
Habari ID: 3476102
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya kuhifadhi Qur’ani yamezivutia familia nyingi huko Al-Quds (Jerusalem), katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Mashindano hayo yanaitwa "Familia ya Qur'ani", yanalenga kuhimiza familia kuhifadhi Qur'ani, Al-Jazeera iliripoti.

Mashindano yalianza tarehe 1 Septemba chini ya usimamizi wa Kituo cha Kuhifadhi na Kufundisha Qur'ani  cha Zayd ibn Thabit na kwa usaidizi wa Al-Quds TV.

Washindani hushindana katika viwango vinne kwa vikundi tofauti vya umri wa miaka 5 hadi 7, 8 hadi 11, 12 hadi 14, na 15 na zaidi.

Shindano hilo litahitimishwa mwishoni mwa mwezi wa Novemba na washindi watapata zawadi za fedha taslimu na vyeti vya heshima.

Katika mfululizo wa hivi punde zaidi wa shindano hilo, lililofanyika Jumamosi na Jumapili, watu wapatao 600 walishindania tuzo ya juu katika kategoria tofauti.

Walijumuisha watoto wenye umri wa miaka mitano kwa mshindani aitwaye Hayat Ghazawi ambaye ana umri wa miaka 72.

Abdul Rahman Bakirat, mkurugenzi wa Kituo cha Zayd ibn Thabit, alisema ni mashindano ya kwanza ya Qur'ani ya aina yake ambayo yanalenga familia.

Alipongeza mapokezi mazuri ya shindano hilo na familia za Wapalestina katika mji huo mtakatifu.

Palestinians in Al-Quds Compete in ‘Quranic Family’ Contest

Palestinians in Al-Quds Compete in ‘Quranic Family’ Contest

Palestinians in Al-Quds Compete in ‘Quranic Family’ Contest

3481269

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha