Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo Alkhamisi wakati alipoonana na washiriki wa Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaliyofanyika hapa Tehran na kuongeza kuwa, mafundisho ya Qur'ani Tukufu yanatuwajibisha kuwatendea wema wanadamu wengine na kuzisaidia jamii za wanadamu.
Amewalaumu viongozi wa nchi za Kiislamu kwa kushindwa kutekeleza kivitendo mafundisho ya Qur'ani Tukufu kuhusu Palestina na kusema kuwa, leo hii vikosi vya wanamapambano wa Kiislamu katika Ukanda wa Gaza vimesimama kidete kupambana na adui khabithi Mzayuni. Amebaini kuwa wanamapambano hao Wapalestina wanafanya hivyo ili kutekeleza kivitendo mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kwa taufiki ya Allah, ushindi utakuwa ni wa taifa la Palestina.
Ameongeza kuwa, bila ya shaka yoyote Ulimwengu wa Kiislamu utashuhudia kwa macho yake namna donda ndugu la kensa la Kizayuni linavyoangamia.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, suala la Gaza ndiyo kadhia kubwa ya Ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa na kuongeza kuwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu atakwenda kuwauliza wananchi Waislamu ambao wameshindwa kuwashinikiza viongozi wao, kama ambavyo viongozi wa nchi za Waislamu nao watakwenda kuulizwa kwa nini walishindwa kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu kuhusu Gaza
Aidha amesema, leo hii Ulimwengu wa Kiislamu na watu huru duniani wanaomboleza mateso wanayoyapata watu wa Gaza.
Amesisitiza kuwa, wananchi wa Gaza wanadhulumiwa na watu ambao hawana chembe ya ubinadamu, ndio maana jukumu kubwa la kila mtu hivi sasa ni kuwasaidia na kuwaunga mkono wananchi madhlumu lakini mashujaa wa Gaza na mapambano yao.
3487300