IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Waislamu Wahimizwa Kufungua Mioyo kwa Mafundisho ya Qur'ani

14:37 - February 24, 2024
Habari ID: 3478406
IQNA – Mtaalamu wa Qur’ani wa Syria amesisitiza kuwa kusoma Qur’ani haitoshi kwani Waislamu wanapaswa kufungua nyoyo zao kwa mafundisho ya Kitabu hicho Kitukufu.

Imad Rami, ambaye alikuwa mjumbe wa jopo la waamuzi katika Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yaliyomalizika Jumatano, aliyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), akisikitika kwamba baadhi ya Waislamu wanaisikia Qur'ani kwa masikio yao lakini wanashindwa kuisikia kwa mioyo yao.

Aliwataka wale wote ambao wamejitolea kwa ajili Qur'an kutafakari aya na mafundisho yake.

Rami alibainisha zaidi kwamba ameshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika nchi 27 kama mjumbe wa jopo la majaji.

Pia amesafiri katika nchi kadhaa kushiriki katika Ibtihal (kusoma dua) katika nchi kadhaa.

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuhudumu kama jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ingawa alisafiri hadi Iran kuhukumu tukio jingine la kimataifa la Qur'ani lililoandaliwa na Al-Kawthar TV.

Mtaalamu huyo wa Syria alisifu ubora wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran na kusema washindani na waamuzi walikuwa wazuri sana.

"Sijaona mashindano ya (Quran) yakifanyika kwa kiwango kama hiki katika nchi zingine," alisema.

Rami pia aliulizwa kuhusu shughuli za Qur'ani nchini Syria. Amesema shughuli hizo zimekua kwa kiasi kikubwa hasa katika miaka ya hivi karibuni baada ya kumalizika vita katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yalifanyika Tehran tarehe 18-24 Februari kwa kushirikisha wasomaji na wahifadhi 69 kutoka nchi 44.

Soma zaidi:

Washindi wa kategoria tofauti katika sehemu za wanaume na wanawake walitajwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga iliyofanyika Jumatano jioni.

Hafla hiyo ya kila mwaka inayoandaliwa na Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada ya Iran, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

3487310

Habari zinazohusiana
captcha