IQNA

Qur'ani Tukufu

Wahifadhi Qur'ani, wasomaji waenziwa katika kambi ya wakimbizi Gaza

6:03 - April 08, 2024
Habari ID: 3478650
IQNA - Kundi la wahifadhi na wasomaji Qur'ani wamehitimu kozi ya Qur'ani iliyofanyika katika kambi moja ya wakimbizi huko Gaza.

Wahitimu hao walitunukiwa zawadi katika hafla iliyoandaliwa katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Programu ya ufundishaji wa kuhifadhi na kusoma Qur'ani katika kambi hiyo ilikuwa maarufu sana miongoni mwa wasichana wadogo.

Kozi hizo zilifundishwa na walimu wa kujitolea wa Qur'ani.

Licha ya utawala haramu wa Israel kuendeleza  vita dhidi ya Gaza na sambamba na jinai zingine nyingi dhidi ya  Wapalestina wasio na hatia, na kuzingirwa eneo hilo la pwani ambalo sasa linakabiliwa na baa la njaa, shughuli za Qur'ani zimeendelea katika eneo hilo.

Watu wa Gaza kutoka rika zote wanasisitiza haja ya kuendelea kujifunza Qur'ani na kuihifadhi licha ya hali ngumu.

Mmoja wa wahifadhi waliotunukiwa katika sherehe hizo alisema Wapalestina wataendelea kufuata nyayo za baba zao na mashahidi wa Palestina.

Vita vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza vilivyoanza tarehe 7 Oktoba 2023 vimesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 33,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na wengine wengi kujeruhiwa.

4208980

Habari zinazohusiana
captcha