Kanisa la Dominicus la Amsterdam Jumapili liliandaa ibada hiyo ya ukumbusho, iliyokuwa na usomaji wa aya za Qur'ani Tukufu.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Meya wa Amsterdam Femke Halsema na Balozi wa Palestina nchini Uholanzi Ammar Hijazi, ililenga kutoa nafasi ya maombolezo na tafakari ya jumuiya.
Akitaja jinsi katika mwaka uliopita wote wamekuwa wakishuhudia mauaji ya kimbari Gaza, Janneke Stegmen, kasisi wa kanisa hilo, alisema: "Tumeona ni muhimu kutoa mahali ambapo watu wanaweza kueleza hisia zao na kuhuzunika pamoja."
Ibada hiyo ilijumuisha wasemaji kutoka imani za Kiislamu, Kiyahudi na Kikristo, ikionyesha hali ya mtangamano wa maswala ya mzozo huo.
Stegmen alisifu ushiriki wa watu wa Imani tofauti katika hafla hiyo na kusema mauaji ya halaiki huko Gaza yamewakera watu wa dini zote tofauti.
Stegmen alisisitiza jinsi ilivyo ngumu kuelewa hali inayoendelea katika Ukanda wa Gaza, akisema: "Hakuna huruma inayoweza kuwa ya kutosha kwa wahasiriwa huko Gaza. Ni changamoto kubwa kushuhudia mauaji haya ya kimbari."
Israel ilianzisha mashambulizi yake ya mauaji ya kimbari ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, baada ya Hamas kutekeleza operesheni ya kihistoria dhidi ya utawala huo katilia ili kulipiza kisasi dhulma zinazozidi kufanywa na utawala huo dhidi ya watu wa Palestina.
kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza , Utawala wa Israel hadi sasa umewaua Wapalestina wasiopungua 42,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi wengine 97,303.
Israel pia imekuwa ikilenga kwa makusudi shule, misikiti na hospitali za eneo lote la Gaza ambalo ambalo imelizingira.
Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeanza kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini kuhusu mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel huko Gaza. Mahakama hiyo imeamuru Israel isitishe mauaji hayo ya kimbari lakini utawala huo wa Tel Aviv umekaidi amri hiyo.
3490170