IQNA

Watetezi wa Palestina

Waandamanaji wanawake Washington DC wabainisha mshikamano na Gaza

19:06 - March 09, 2024
Habari ID: 3478472
IQNA - Wnawake wanaharakati wanaounga mkono Palestina wameandamana katike eneo la Freedom Plaza katika mji mkuu wa Marekani, Washington, DC, kutangaza mshikamano na wanawake wa Kipalestina wanaoteseka huko Gaza, huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza mauaji ya kimbari katika eneo hilo.

Maandamano hayo yaliandaliwa siku ya Ijumaa, kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Maandamano hayo yaliyoratibiwa na Harakati ya Vijana wa Palestina yalikuwa ni kuashiria hali mbaya ambayo wanawake na watoto wa Gaza wamekuwa wakikabiliana nayo na kutaka kusitishwa mara moja mauaji ya kimbari na uungaji mkono wa kijeshi wa Marekani kwa utawala dhalimu wa Israel.

Miranda Dube, kutoka Harakati ya Vijana wa Palestina, alisema wanawake wa Palestina "wako mstari wa mbele katika vita" tangu kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya Gaza mwezi Oktoba.

"Wanawake wanalazimishwa kujifungua chini ya hali ya kutisha na mazingira machafu," alisema. “Kumekuwa na watoto 20,000 ambao wamezaliwa tangu Oktoba 7. Bila uangalizi mzuri, watoto wanakufa kwa njaa, akina mama wanashindwa kuhudumia watoto wao.

"Tupo hapa kwa sababu huwezi kuwa na siku ya kusherehekea wanawake bila kuelewa kuwa mfumo dume kwa asili umefungamanishwa na ubeberu na unahusishwa na Uzayuni," aliongeza.

Layla Summers, 45, kutoka jimbo la California, alisema ujumbe wake kwa Rais wa Marekani Joe Biden na wanasiasa wote ni kwamba wanawake wa Gaza pia ni wanadamu na kuongeza kwamba  akina mama wa Gaza wanaopoteza watoto wao na wanatazama watoto wao wakifa kwa njaa."

Takriban wanawake 8,900 wameuawa huko Gaza tangu vita vya Israel dhidi ya eneo hilo kuzuka Oktoba 7, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Gaza ilisema Ijumaa.

Kwa ujumla, zaidi ya Wapalestina 30,800 wameuawa na zaidi ya 72,400 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel yanayoendelea Gaza huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji.

Makundi ya Wapalestina yanakadiria kuwa maelfu ya Wapalestina wamekamatwa na wanashikiliwa katika jela za kuogofya za jeshi Israel.

Israel pia imeweka vizuizi kwenye eneo la bahari, na kuwaacha wakazi wake, haswa wakaazi wa kaskazini mwa Gaza, kwenye hatihati ya njaa.

Vita vya Israel dhidi ya Gaza  vimesukuma asilimia 85 ya wakazi eneo hilo kuhama makazi yao huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, huku asilimia 60 ya miundombinu ya eneo hilo ikiharibiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Uamuzi wa muda wa mwezi Januari uliiamuru Tel Aviv kusitisha vitendo vya mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba msaada wa kibinadamu unatolewa kwa raia huko Gaza.

3487479

Habari zinazohusiana
captcha