IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Vikao vya Qur'ani Tukufu vimepangwa katika Chuo Kikuu cha Ahl-ul-Bayt (AS) mwezi wa Ramadhani

17:47 - February 28, 2023
Habari ID: 3476638
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Baraza la Dunia la Ahl-ul-Bayt (AS) alisisitiza haja ya kuandaa vikao vya Qur’ani katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Ahl-ul-Bayt (AS) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hujjatul Islam Saeed Jazari Ma'amouei Jumatatu alihutubia hafla iliyofanyika chuo kikuu kusherehekea Idi za Sha'aban.

Katika hotuba yake, Hujjatul Islam Saeed Jazari Ma'amouei aliwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo kikuu.

Vile vile ameashiria fursa ambayo mwezi mtukufu wa Ramadhani hutoa kwa shughuli za Qur'ani kama vile vikao vya Qur'ani Tukufu, programu za kufundisha Qur'ani, vipindi vya Tafsir na matukio mengine.

Alisema programu hizo zinakuza mazingira mazuri ya Qur'ani Tukufu katika chuo hicho, ambayo yatakuwa na matokeo mazuri sana ya kiroho.

Khatibu huyo ameongeza kuwa miezi ya Hijria Qamari ya Rajab, Sha’aban na Ramadhani ni fursa kwa mtu kujielimisha Nafsi na kupata fadhila za kiroho.

Kila mwaka, sherehe mbalimbali hupangwa sehemu mbalimbali za dunia kwa mnasaba wa kumbukumbu za kuzaliwa Imam Hussein (AS), Hazrat Abbas (AS) na Imam Sajjad (AS), ambazo mtawalia zimeangukia tarehe 3, 4 na 5 za mwezi wa Sha'aban (Februari 24, 25, 26 mwaka huu).

Waislamu pia wanaadhimisha siku ya 15 ya mwezi wa Sha'ban (Machi 8, mwaka huu) ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe ujio wake).

Ramadhani (inayotazamiwa kuanza Machi 23 mwaka huu) ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu ambapo Waislamu hufunga kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi Magharibi. Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) katika mwezi huu.

Habari zinazohusiana
captcha