IQNA

Mashindano ya Qur’ani yafanyika Palestina

23:57 - July 26, 2016
Habari ID: 3470476
Mashindano ya kitaifa ya kusoma Qur’ani kwa kuzingatia misingi ya Tajweed yamefanyika Palestina kuanzia Julai 24.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Palestina, washichana na wavulana wapatao 3,000 kutoka maeneo yote ya Palestina wameshiriki.

Sheikh Yusuf Id’is, Waziri wa Awqaf na Masuala ya Kiislamu Palestina, amesema kushiriki idadi kubwa ya wanafunzi katika mpango huo ni ishara ya namna Qur’ani Tukufu ilivyo na umuhimu katika utamaduni wa Wapalestina.

Amesedma wizara yake inapanga kufungua vituo Zaidi vya kutoa mafundisho ya Qur’ani ili kuhakikisha kunakuwepo kizazi chenye kuzingatia misingi ya Uislamu katika siku za usoni.

Aidha amesema Wapalestina wamepataza zawadi nyingi katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani katika nchi kadhaa duniani.

/3517423

Kishikizo: palestina qurani iqna
captcha