IQNA

Kituo cha Qatar ni Kitovu Kikuu cha Shughuli za Qur'ani kwa Wanawake

21:33 - May 23, 2023
Habari ID: 3477036
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Kamila al-Kuwari ni kitovu kikuu cha shughuli za Qur'ani kwa wanawake katika mji mkuu wa Qatar, Doha.

Kituo hicho kilizinduliwa mwaka wa 2016 katika jengo la wakfu katika wilaya ya al-Kharitat katika kitongoji cha Doha na kinafanya kazi chini ya usimamizi wa Idara ya Dawah (kuhubiri) na Mwongozo wa Kidini.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar hivi karibuni ilitoa ripoti kuhusu shughuli za kituo hicho.

Kwa sasa, wanawake na wasichana 492 katika vikundi vya umri tofauti wanajifunza Qur'an kwa moyo katika kituo hicho, ripoti hiyo ilisema.

Wanafundishwa na walimu 17 wa kike wa Quran, ilisema.

Imeongeza kuwa programu na shughuli za kituo hicho zinatekelezwa kwa kuzingatia mipango ya wizara ya kuendeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu na maadili ya Kiislamu katika jamii.

Kulingana na mkurugenzi wake, Nour al-Kabisi, kituo hicho kimepewa jina la Kamila al-Kuwari, mwanamke ambaye alikabidhi jengo hilo mnamo 2016.

4142614

Kishikizo: qatar qurani
captcha