IQNA

Mayahudi katika Qur'ani / 3

Tofauti kati ya Myahudi na Mzayuni

17:09 - June 01, 2024
Habari ID: 3478913
IQNA - Mzayuni ni Myahudi ambaye ana imani ya kufurutu ada kuhusu 'ubora wa juu zaidi' wa watu wa Mayahudi na kwamba warejee katika kile wanachodai ni  "Nchi Ya Ahadi".

Hatahivyo  Yahudi wa kweli ni yule ambayo  anafuatilia tafsiri sahihi Torati na kutenda kwa mujibu wa Sharia ya Nabii Musa (AS).

Uyahudi ni dini ya Mwenyezi Mungu ambayo wafuasi wake wanaamini utume wa Musa na wanaichukulia Torati kuwa ni kitabu chao kitakatifu.

Wale walioamini dini ya Kiyahudi walijua kwamba dini hiyo ndiyo imani rasmi ya kimungu mpaka Mungu atakapomtuma mjumbe wake mwingine. Wafuasi wa dini ya Kiyahudi walifungamana na kanuni na sheria zilizotajwa katika Torati. Hata hivyo, katika kipindi cha historia, baadhi ya watu waovu  waliipotosha kwa manufaa yao binafsi na ya kidunia.

Sayuni (Zion) ni jina la mlima karibu na al-Quds (Jerusalem) ambao ulikuwa mahali pa ibada miongoni mwa Wayahudi wachamungu kwa karne nyingi. Watu hao waliitwa Wazayuni. Hata hivyo, maana ya neno hilo ilibadilika kabisa katika karne ya 19 na wanasiasa wa Kiyahudi walitathmini maana mpya ya Wazayuni kuwa mkondo wa kisiasa na kiitikadi wa kurudi katika nchi ya ahadi.

Tangu wakati huo, wale ambao, kwa kuzingatia ngano, ambazo si sahihi, wanaamini kuhusu kulekea Mayahudi  huko Palestina na kuanzishwa kwa dola ya Kiyahudi walitambuliwa kama Wazayuni. Hapo awali baadhi ya viongozi wa Kizayuni hawakuwa na imani na Mwenyezi Mungu, huku baadhi ya wafuasi wao wakiamini kwamba kufukuzwa kwa Wayahudi sio matokeo ya dhambi zao bali ni kwa sababu ya idadi yao ndogo.

Hata hivyo, baadaye walisisitiza kwamba taifa la Kiyahudi lilipaswa kuasisiwa mahala fulani kwa kutumia mafundisho ya kidini na mbinu za kisiasa. Kwa hivyo kwa mtazamo mmoja, Uzayuni unaweza kuzingatiwa kama aina fulani ya tafsiri ya kisiasa ya Torati.

Kwa ujumla, Mzayuni anaweza kufafanuliwa kama Myahudi ambaye anaamini kuhusu 'ubora wa juu zaidi' wa Mayahudi na anazingatia kurudi kwenye "nchi ya ahadi" ya Al Quds (Jerusalem) kama haki na wajibu wake na anafanya kila kitu kwenye njia hii. Na anachotaka kufikia kwa kurejea katika ardhi hii ni kuitawala dunia na kisha kutawala kibeberu mataifa mengine yote duniani. Na hii ndiyo nukta iliyotajwa katika Qur'ani Tukufu. Hivyo iwe Wayahudi hao wabaguzi wanaishi katika karne zilizopita au wakati wa sasa, wanaifanyia kazi Torati iliyopotoshwa. Hii ni katika hali ambayo Wayahudi wa kweli wanafuata tafsiri sahihi ya Torati na kutekeleza mafundisho ya Musa (AS).

Uzayuni wa kisasa una chimbuko lake katika utaifa na ukoloni wa Ulaya wa karne ya 19. Katika upande mwingine Wayahudi wanaotafuta ukweli unaotegemea Torati wanapinga Uzayuni wa leo.

Ili kuwajua Wazayuni, cha kutilia maanani zaidi sio dini au rangi bali tabia na sera, misingi ya utambulisho na mwenendo.

Ndiyo maana tunashuhudia kuibuka kwa Wazayuni wa Kikristo nchini Marekani (wakati wa uongozi wa George W. Bush) na kuibuka kwa aina ya Uzayuni wa Kiarabu katika miaka ya hivi karibuni. Hata rais wa sasa wa Marekani, ambaye ni Mkristo, amewahi kujitambulisha mara kadhaa kama Mzayuni. Hata hivyo, Wazayuni walioibuka hivi karibuni hawana mielekeo ya kutekeleza Torati asili  na hawawaoni Mayahudi kuwa ni jamii bora zaidi bali wanaweza kuitwa Wazayuni kwa sababu tu ya kuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel na ukandamizaji pamoja na ukaliwaji mabavu ardhi za Palestina.

3488398

captcha